Nabii Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie leo ametunukiwa shahada ya Udaktari wa heshima na tuzo ikiwa ni kumuheshimisha kutokana na mambo mengi anayofanya katika kuisadia jamii.
Tukio hilo limefanyika katika ukumbi wa Sephil Saphire mnamo julai 5, 2025 mjini Dodoma kuanzia majira ya saa tatu asubuhi hadi saa Saba mchana na limeandaliwa na umoja wa Chama Cha Madaktati na Maprofesa Tanzania.
Akizungumza baada ya kutunukiwa shahada hiyo ya falsafa ya
udaktari Nabii Mkuu Mke. Dkt. GeorDavie amesema umempa hamasa kubwa na msisimko
mpya wa kuendelea kuisaidia jamii na kushughulika na mahitaji mbalimbali ya
watu katika kuleta maendeleo kwa ujumla.
Akizungumza mara baada ya kumtunuku shahada hiyo mgeni
rasmi ambaye pia ni Mwenyekiti wa umoja wa Chama Cha Madaktati na Maprofess,
Prof. Rejoice Ndalima amesema kuwa Nabii Mkuu amestahili kwa sababu amekuwa
akisaidia wananchi bila kubagua.
Aidha tukio hilo kubwa na la kihistoria limehudhuria na
Madaktati na Maprofesa wa hapa nchini, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na
Amani Taifa, watumishi wa Mungu pamoja na watu kutoka mikoa mbalimbali hapa
nchini.
Na Beatrice Maina@NYU ARUSHA.
No comments:
Post a Comment