Wednesday, August 30, 2017

LIVERPOOL KUMSAJILI OXLADE CHAMBERLAIN.

Liverpool imekubali kuilipa Arsenal dau la £40m kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Alex Oxlade Chamberlain.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye alikataa uhamisho wa Chelsea siku ya Jumanne baada ya makubaliano kuafikiwa, atajiunga na Liverpool kwa kandarasi ya miaka mitano ambapo atakuwa akipokea £120,000 kwa wiki.
Liverpool imekubali kuilipa Arsenal dau la £40m kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Alex Oxlade Chamberlain
Oxlade Chamberlain ambaye yuko mwaka wake wa mwisho wa
kandarasi na Arsenal, alikataa mkataba mpya ambao angekuwa akilipwa £ 180,000 kwa wiki katika uwanja wa Emirates.
Ameanzishwa mechi zote nne za Arsenal msimu huu.
Kiungo huyo wa kati anatarajiwa kufanyiwa ukaguzi wa matibabu kabla ya kuelekea Malta na Uingereza siku ya Alhamisi kabla ya dirisha la uhamisho kukamilika.
Oxlade Chamberlain ameichezea klabu hiyo mara 198 tangu ajiunge naye kutoka Southampton mnamo mwezi Agosti 2011, akifunga mabao 20.
Kitita hicho kingevunja rekodi ya usajili wa Liverpool, lakini timu hiyo imekubali kumsajili mchezaji wa RB Leipzig Naby Keita msimu ujao kwa kitita cha £48m.
Kufikia sasa Liverpool imemsajili winga Mohammed Salah kutoka Roma kwa £34m, beki Andrew Robertson kutoka Hull kwa £8m na mshambuliaji Dominic Solanke baada ya kandarasi yake katika klabu ya Chelsea kuisha.

No comments:

Post a Comment