Thursday, August 31, 2017

KUWENI NA IMANI KWA MUNGU.



        BALOZI WA NABII MKUU TANZANIA MTUME SEKELA N'TONDOLO

watu wametakiwa kuwa na imani kwa mungu kupitia watumishi wake anaowatumia kwani itawasaidia kufanikiwa katika mambo  mbalimbali maishani .


hayo yamesemwa na balozi wa nabii mkuu tz mtume sekela n'tondolo wakati akihubiri katika ibada ya chuo cha manabii liyofanyika hii leo alhamisi tarehe 31/08/2017 kwenye chuo kikuu cha manabii ambapo alifundisha somo lililokuwa na kichwa kisemacho jinsi ya kuhamisha milima kiimani.

            BAADHI YA WATU WALIOSHIRIKI IBADA HIYO YA CHUO CHA MANABII SI

 amesema kuwa kufanikiwa huko ni kupitia matamko mbalimbali yatolewayo na watumshi wa mungu ambapo kama mtu akikiri basi lazima afanikiwe kwani imani ni jambo zuri sana lenye kumfurahisha mungu.

 somo alilofundisha lilitoka marko 11:23
"amini nawaambia yeyote atakayeuambia mlima huu ng'oka ukatupwe baharini  wala asione  shaka moyoni mwake ila amini kwamba hayo asemayo yametukia yatakuwa yake"

No comments:

Post a Comment