Thursday, May 10, 2018

KAULI CHANYA AMBAZO HUTASIKIA POPOTE KUHUSU ''MATATIZO /MAKOSA''

Nashindwa hata niongelee vipi neno tatizo.Sababu kila mmoja ana maana yake.Na matatizo yanatofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu.Familia hadi familia,ukoo hadi ukoo,jamii hadi jamii.na taifa hadi taifa.Nchi za dunia ya tatu zikiwa na matatizo ya maji safi na barabara nzuri.Mataifa ya dunia ya kwanza yanapitia makosa kadhaa ili kutafta amani  ya milele na upendo wa kweli.Jamii ya wafugaji ikiwa na tatizo la ardhi kwa matumizi ya mifugo  na wanyama.Jamii ya wakulima inapitia makosa kadhaa ili kupata ardhi kwa matumizi ya mazao na mashamba.Sote kwa nyakati mbalimbali tunakumbwa na shida zisizoligana.Tunatenda makosa yasiofanana.Na muda mwingine tunakuwa hivi kulingana na athari hasi ya mafunzo tuliyopata. Tulifundishwa shule,mwenye akili ni yule asiyekuwa na matatizo  ni yule asiyefanya makosa.Mwenye vema nyingi za zoezi ni mshindi.Mwenye maksi kubwa za mtihani ni wa kwanza.Mwenye makosa mengi ni mjinga ni wa mwisho hata baada ya masahihisho picha hiyo haibadiliki kwa huyo mtu.Tuliaminishwa hivyo tukasadiki hivyo.Kumbe hata kuamini hivyo kwa asilimia 100 ni makosa bado.Kwa sababu mambo yanakawa kinyume tunapoingia mitaani.Huku anayekosea sana na kujisahihisha ndiye mshindi, ndiye anayesogelea mafanikio ndiye anayeitwa tajiri.Hakuna tajiri aliye na stori ilinyooka.Kuna mahala alishindwa ,alikatishwa tamaa,aliogopa  lakini akapiga moyo konde na kuendelea. Umewahi kumsikia.Edson Thomas aliyefanya majaribio ya taa 10,000 bila mafanikio.Taa ya 10,001 ndio ikamletea heshima na utajiri.Au umewahi kusikia stori ya Abraham Lincolin,Rais wa marekani aliyeshindwa biashara tatu wakati wa ujana, akapigwa chini  mara saba katika  kampeni wakati wa kutafta nyasifa za kisiasa?.  Mpaka baadae ndipo anakuwa rais wa awamu ya 16 ya  hilo taifa lenye nguvu duniani.Hivyo hatuna haja ya kuogopa kukosea kwani haya maisha yanaturejesha kwenye maana mpya kabisa ya neno tatizo au matatizo. kosa au makosa.
1.''Kama hujawahi kukosea hujawahi kujaribu kitu kipya'' Albert Einstain

2.''Makosa ni kiashiria cha ukomo wa maarifa yako''Robert Kiyosaki


3.''Matatizo ni kipimo cha mtu na akili''Luther king jr

4.''Kila mbele ya tatizo kubwa pana fursa njema inakusubiri''

5.kukimbia tatizo hakulitatui bali kunaongeza umbali kati ya tatizo na utatuzi
6.Mwanvuli haukati mvua ispokuwa unatupa ujasiri wa kusimama katikati ya mvua,matatizo hayakwazi maisha isipokuwa yanatupa utashi wa kujikwamua.
7.Tatizo ni sawa na mashine ya nguo katika kazi na madadiliko,tegemea  kufikichwa,kukunjwa,kusuguliwa mpaka uwapo safi zaidi ya ulivyokuwa hapo  mwanzo
8.Tatizo ni sawa na dirisha litakupa upeo wa mbali endapo utalisogelea.

9.Matatizo ni kipimo unahitaji mafanikio kiasi gani.Unavyoyatatua mengi, mafanikio yako yanaongezeka.
 
by rich voice

No comments:

Post a Comment