Tuesday, May 1, 2018

Hii ndio idadi ya watumishi serikali inayotarajia kuwaajiri



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa tangu aingie madarakani wameajiri jumla ya watumishi 18,101 katika sekta mbalimbali nchini.

Akizungumza leo Mei 1 mkoa Iringa katika siku ya Wafanyakazi ambapo amesema jumla ya watumishi 22,150 wanatarajia kuwaajiri.

“Tangu tuingie madarakani tumeajiri watumishi wapya 18,101 wakiwemo walimu zaidi ya 6,500, watumishi wa afya 3,752, watumishi wa mambo ya ndani (polisi, magereza, uhamiaji) 6,164,“ amesema
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa kabla ya mwaka huu wa fedha kumalizika inatarajia kuajiri watumishi 22,150.

CHANZO -THE RICH VOICE

No comments:

Post a Comment