Friday, May 4, 2018

Dhlakama kiongozi wa RENAMO afariki

Afonso Dhlakama 

Chama cha Upinzani nchini Msumbiji kimesema kuwa kiongozi wake wa muda mrefu Afonso Dhlakama amefariki dunia kwa ugonjwa wa moyo, akiwa na miaka 65.

Dhlakama aliiongoza RENAMO katika kipindi cha miaka 15 ya uasi dhidi ya serikali ya Msumbiji, kilichomalizika mwaka mwaka 1992.
Alikuwa akiungwa mkono na serikali iliyokuwa ikiongozwa na Wazungu nchini Afrika kusini na baadaye kuja kuwa Rhodesa.
Chama cha Renamo kilikuwa kikilaumiwa kwa mauaji ya watu wengi, kuwatumia watoto vitani.
Baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, Renamo kikawa chama kikuu cha upinzani nchini Msumbiji.
Wafuasi wake wameendelea kupambana na majeshi ya serikali.
chanzo- bbc swahili


No comments:

Post a Comment