Thursday, May 10, 2018

MBUNGE WA MBEYA MJINI MH. JOSEP MBILINYI “SUGU” AACHIWA HURU LEO


index
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wakilakiwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mh. Freeman Mbowe mara baada ya kuachiwa huru leo Alhamis Mei 10,2018 jijini Mbeya.
Awali Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda na viongozi wengine wa chama hicho wamefika Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya kuwapokea Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga.
Wawili hao wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao
Akihojiwa na kituo cha Redoa cha Clouds Mwenyekiti wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe amesema wamepata taarifa kutoka vyanzo vyao ambavyo hakuvitaja kwamba Mh. Joseph Mbilinyi anaachiwa leo asubuhi kutoka Gereza la Ruanda ambako alikuwa akitumikia kifungo cha Miezi mitano na mwenzake Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga
Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
 
by richard shiyo/rich voice

No comments:

Post a Comment