Thursday, May 10, 2018

Serikali yaja na Mbinu mpya kudhibiti wizi wa bili za maji na wakwepaji kodi

Katika kuongeza mapato kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Arusha na kupunguza malalamiko ya wananchi ya kulalamikia kuibiwa pindi wanapolipa bili ya maji serikali ya halmashauri hio chini ya Shirika lisilo la kiselikari lijulikanalo kwajina la Water aid limeunda mfumo mpya wa upatikanaji wa maji ujulikanao kwa jina la e water ambao utadhibiti mianya ya ukwepaji kodi

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Dr Charles Mahela kwenye uzinduzi wa semina ya maji ilio andaliwa na Shirika la Water aid ambalo linahusika na mradi huo wa e water ambao umegarimu takribani shilingi milioni 800
Hata hivyo wataalamu washirika hilo wameeleza namna mfumo huo unavyofanya kazi nakusema kua njia hio itaimarisha ukusanyaji wa mapato pia nirahisi katika kusaidia mamlaka husika katika zoezi la uendeshaji wa huduma hio
Pia meneja wa mamlaka ya maji katika mji mdogo wa Ngaramtoni ndugu Grayson kimaro amesema kua hali ya huduma ya maji inaendelea kuimarika siku hadi siku.
by rich voice

No comments:

Post a Comment