Thursday, February 12, 2015

IBADA YA CHUO CHA UPONYAJI TAREHE 12/February/2015.



Nabii Mkuu Mh.Dr.GeorDavie ametoa Unabii wa Muda wa miezi mitano kuanzia Februari hadi June mwaka huu kuwa kuna mambo yatakayotokea ambayo yatakuwa ya kushangaza. Mh.Dr.GeorDavie ametoa Unabii huo leo wakati wa ibada ya Chuo cha Uponyaji iliyofanyika katika hema la Kukutania la Ngurumo ya Upako Chuo Kikuu cha Manabii  Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.Akitoa unabii huo amesema kuwa kuanzia mwezi huu kuna vikao fulanifulani vya mashetani vinavyodai damu za watu lakini watu wanaomwamini Nabii watakuwa salama. 

Katika ibada hiyo iliyohudhuriwa na watu kutoka ndani na nje ya jiji la Arusha ambao waliweza kufunguliwa kutoka kutoka katika vifungo mbalimbali vya nguvu za giza huku wengine wakitamkiwa maneno mbalimbali ya Unabii.
Pamoja na mambo mengine Nabii Mkuu amewatamkia watu wote wanaoamini nguvu ya Kinabii kuwa Mungu amewatua mizigo yote na wako huru kabisa kukaa katika imani sahihi na Neno la Mungu.

Nabii Mkuu Mh.Dr.GeorDavie atakuwepo katika ibada ya chuo cha uponyaji Alhamisi Ijayo ya februari 19 katikia hema la Kukutania la Ngurumo ya Upako Chuo Kikuu cha Manabii ambapo amesema kuja kwake si bure bali ni kwa sababu ya vitu ambavyo Mungu amemuonye kwa ajili ya watu wake.