Monday, February 16, 2015

IBADA YA JUMAPILI.TAREHE 15/February/2015




Baraka mbalimbali za kinabii zimeendelea kumiminika kwa Maelfu ya watu walioudhuria ibada ya Jiji Chuo Kikuu cha Manabii Kisongo nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Katika ibada hiyo Nabii Mkuu Mheshimiwa Dr GeorDavie  ametangaza Baraka mpya ya
jambo jipya huku maelfu ya watu wanaoamini nguvu ya Kinabii wakiendelea  kutembea  na neno la  siku 14 za kupokea wazo la Kimungu katika shunguli mbalimbali  sambamba na kutamkiwa uponyaji pamoja na upenyo katika mambo mbalimbali.

Katika ibada hiyo Nabiii Mkuu amefundisha juu  ya Tathimini ya Ukuaji na Maendeleo ya muumini huku akisisitiza kuwa kila jambo mtu analolifanya lazima atathmini sababu ya kuwa baya au zuri.

Mbali na hayo Dr.GeorDavie ameitaka jamii kuwa na matumizi mazuri ya fedha kwa kuweka akiba, malengo hasa wakati wakutekeleza masuala mbalimbali hasa wakati wa kuchukua mkopo na kuhakikisha kuwa unatumika katika mipango iliyokusudiwa.