Thursday, February 5, 2015

HUDUMA YA NGURUMO YA UPAKO ILIYOKO CHINI YA NABII MKUU MH.DR.GEORDAVIE IMETOA MSAADA KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI KUMI .



Huduma ya Ngurumo ya Upako iliyoko chini ya Nabii Mkuu Mh.Dr.GeorDavie leo imetoa msaada kwa vituo sita vya watoto yatima wenye thamani ya shilingi milioni kumi .

Msaada huo ambao ni vitu mbalimbali kama Mchele, sukari, mafuta ya kupikia pamoja na sabuni umekabidhiwa kwa walezi wa vituo hivyo lengo likiwa ni kuwasaidia watoto hao ili nao wajione kuwa sawa na watoto wengine wenye wazazi.

Akikabidhi misaada hiyo kwa niaba ya Nabii Mkuu, Kadinali wa Kwanza wa Huduma ya Ngurumo ya Upako Mtume Gaudensia Luila amesema kuwa misaada hiyo ni kutimiza neon la bwana.

Akipokea msaada huo Mkurugenzi wa kituo cha watoto cha Lohada ameishukuru huduma ya Ngurumo ya upako kwa kumpatia msaada kwa ajili ya watoto.
Kwa upande wao walezi wa vituo hivyo wameonyesha furaha  wakipokea msaada huo huku wakitoa wito kwa jamii, serikali na taasisi mbalimbali kuweza kutoa michango yao ili kuweza kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Aidha vituo vilivyopatiwa msaada huo ni St.John’ Anglican church Group, African Orphanage, New Outlook Center Tanzania, Kindness Children care, Lohada pamoja na kituo cha Christian Women Orphanege Care.

No comments:

Post a Comment