Monday, February 2, 2015

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 2/February/2015


Maelfu ya watu wamekusanyika katika chuo kikuu cha manabii kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha kwenye ibada ya jiji ambayo iliongozwa na Nabii mkuu Dr. GeorDavie na kupokea Baraka mbalimbali za kinabii.
Katika ibada hiyo Nabii Mkuu DR.GAEORDAVIE ametangaza kuwa hii ni wiki ya kupanda ngazi katika maeneo mbalimbali. Nabii mkuu amefafanua kuwa Mungu anapokaa ndani ya mtu hakubaliki,na pia ni vigumu kueleweka miongoni mwa watu.
 Dr.GeorDavie Aliendelea kusema kuwa mtu wa Mungu hutambuliwa kwa matunda yake na si kwa wingi wa maneno ya watu wanayosema.

 Aidha Nabii mkuu amebainisha wazi kuwa neno la Mungu pekee ndilo linaloweza kumtakasa mtu katika akili,dhambi na makosa,kwa na namna ambavyo maneno ya Mungu yanavyozidi kuingia ndani ya mtu na ndivyo ambavyo mtu anatakasika siku baada ya siku.

No comments:

Post a Comment