Thursday, January 29, 2015

IBADA YA CHUO CHA UPONYAJI TAREHE 29/January/2015





Maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha na wale wanaoamini Nguvu ya Kinabii  wametengwa na kila kusudi baya la shetani katika mambo mbalimbali maishani.
Hayo yamefanyika katika Chuo Cha Uponyaji katika hema la kukutania la Ngurumo ya Upako Chuo Cha Manabii Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.

Katika ibada hiyo Nabii Mkuu Mheshimiwa Mhe.Dr.GeorDavie amesema kuwa kila jambo baya lililokusudiwa na adui katika nyanja mbalimbali katika maisha ya mtu binafsi,kazi na  familia  wametengwa nayo. 

Sanjari na hayo katika ibada hiyo watu walipita mbele ya Nabii Mkuu Mheshimiwa DR. GEORDAVIE  kama mfano wa kupita katika tanuru la moto wa roho mtakatifu alilolitengeneza  ili kuwatenga na kusudio baya la shetani.

Aidha ameongeza kuwa moto wa roho mtakatifu ni zaidi ya moto ule wa nyumbani kwani  unateketeza kila aina kusudi baya na kuongeza kuwa Mungu amewapa ushindi wale wote wanaomini nguvu ya kinabii  ili waweza kutimiza mipango mikubwa. 

Atengwa kutoka kwenye vifungo vya kishirikina.


No comments:

Post a Comment