Friday, January 23, 2015

IBADA YA CHUO CHA UPONYAJI TAREHE 22/January/2015.





Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Ngurumo ya Upako duniani Nabii Mkuu Mh.Dr.GeorDavie amewabariki maelfu ya watu kwa kuwaingizia kitu cha Kimungu ambacho pia kitawasaidia kumtafuta Mungu.

Hayo yamefanyika katika ibada ya chuo cha Uponyaji iliyofanyika katika hema la Kukutania Chuo Kikuu cha Manabii Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.

Awali Nabii Mkuu alianza kwa kumruhusu Roho Mtakatifu kwa maelfu ya watu waliohudhuria ibada hiyo ambapo amesema Roho Mtakatifu ni mwalimu hutufundisha,hutukumusha, ni mshauri katika njia zetu.


Katika ibada hiyo watu mbalimbali wamepokea uponyaji wa magonjwa mbalimbali huku wengine wakishushwa mizigo waliyokuwa wamebebeshwa kwa neno la Kinabii wamekuwa huru.
Aidha Nabii Mkuu amesema Alhamisi ya wiki ijayo atakuwepo katika chuo cha uponyaji kwa ajili ya kuwatenga watu na kila aina ya uharibifu.
Nabii Mkuu Mh.Dk.GeoDavie akiziundua kalenda ya Huduma ya Ngurumo ya Upako mwaka 2015.