Monday, January 26, 2015

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 25/01/2015.




Jamii nchini imetakiwa kutambua mchango wa wazazi wao bila kujali kiwango cha msaada waliuopata kutoka kwao.

Rai hiyo imetolewa na kiongozi mkuu wa Huduma ya Ngurumo ya Upako Duniani Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie katika ibada ya jiji  Chuo Kikuu cha Manabii Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.    
Nabii Mkuu DR.GEORDAVIE amefafanua kuwa ipo tabia  miongoni mwa watu  kuwalaumu wazazi kuwa hawajawandalia msingi mzuri wa maisha jambo alilosema si sahihi na badala yake kwa kila anaye amini nguvu ya huduma ya Ngurumo ya Upako anaweza kupokea kila anacho kihitaji.


Aidha katika ibada hiyo Nabii Mkuu ametamka maneno mbalimbali ya hekima za kinabii na kusema wakati uwapo katika  nguvu ya  kinabii hupaswi kuwalaumu wazazi hata kama hawakuweza kukusaidia yale ambayo ulihitaji kutoka kwao, badala yake unapaswa kuwashukuru wazazi kwa kukuzaa na pia kuchukua jukumu la  kuwatunza na kuwasaidia kama wazazi wako.

Sanjari na hayo Nabii Mkuu Dr Geordavie alitangaza kuwa wiki hii ni wiki ya wepesi katika majukumu mbalimbali.


No comments:

Post a Comment