Monday, August 24, 2026

MCHUNGAJI KIONGOZI MAMA ANNA DAVIE AWASHUKURU INTERNATIONAL PARTNERS KUENDELEA KUSAPOTI KAZI YA MUNGU

Mchungaji Kiongozi Mama Anna Davie amewashukuru na kufurahishwa na wana international Partner ambao wanatoa fedha zao kwa moyo wakupenda kwa ajili ya kusapoti maono ya Mtu mkuu wa Mungu.

Ameyasema hayo hii leo wakati wa ibada ya chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika nyumba nyumba ya matamko ngurumo ya upako kisongo.

Akizungumza amesema kuwa ni jambo la ajabu mtu kutoa kwa hiari na kwa furaha kwa ajili ya kutimiza kazi ya huduma huku wakitegemea kupokea baraka.

Naye Mtume Elisifa Kephasi akifundisha somo la chagua kwenda mbele sio kurudi nyuma amesema kuwa katika kwenda mbele lazima uchague kwenda na Mungu na sio kundi la watu kwa sababu watu wanaweza kukuacha njiani lakini Mungu hawezi kukuacha.

Kwa upande wake Mchungaji Paulo Mkumbo amesema mtu atakapo liandama agano ambalo Mungu amefanya na Baba wa Kiroho kwa nguvu zote utamuona Mungu katika Maisha yako.

Pia kijana Jackline Kessy amepata nafasi ya kuhubiri ambapo kupitia kichwa cha somo kisemacho KUBALI MCHAKATO WA KUOZA ILI UMEE TENA amesema kuwa ili mbegu iote na kukua lazima ioze na unapokubali kuoza unakubali kuongozeka.



No comments:

Post a Comment