Tuesday, August 11, 2026

KLABU YA FENERBAHCE IMEFIKIA MAKUBALIANO NA NAPOLI YA KUMSAJILI MSHAMBULIAJI, ROMELU LUKAKU

 


Klabu ya Fenerbahce ya Nchini Uturuki imefikia makubaliano na na Napoli ya Italia juu ya kumsajili mshambuliaji, Romelu Lukaku (33) kwa ada ya uhamisho ya euro milioni 6 itakayofikia euro milioni 8 pamoja na nyongeza.

Nyota huyo wa Kimataifa wa Ubelgiji tayari amefikia makubaliano ya maslahi binafsi na klabu hiyo na anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na chaguo la ongezeko la mwaka mmoja zaidi.

Mshambuliaji huyo wa zamani Chelsea na Manchester United anatarajiwa kutia kibindoni mshahara wa Euro milioni 10 (zaidi ya Tsh bilioni 30.5) kwa mwaka.

Miaka mitano iliyopita Chelsea ilimsajili nyota huyo kwa dau la Euro milioni 113 akitokea Inter Milan kabla ya kuuzwa kwenda Napoli kwa dau la Euro milioni 30.7 mnamo Agosti 2024 na sasa anatarajiwa kutimkia Uturuki kwa dau la Euro milioni 8.

No comments:

Post a Comment