Wednesday, August 19, 2026

KICHERE ASISITIZA UMUHIMU WA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATI YA TAASISI ZA UKAGUZI, MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za ukaguzi, mapambano dhidi ya rushwa na udhibiti wa manunuzi ya umma katika kuzuia upotevu wa rasilimali za Serikali na kukabiliana na utakatishaji fedha. 

Ofisi ya CAG ina jukumu la kufanya ukaguzi unaolenga kuimarisha uwazi, uwajibikaji na usimamizi bora wa rasilimali za umma.  

Ameyasema hayo leo jijijini Arusha wakati akizungumza katika mkutano wa mwaka wa 19 wa INTOSAI Working Group on the Fight Against Corruption and Money Laundering (WGFACML) ulioandaliwa na Ofisi ya Taifa ya ukaguzi (NAOT).

Kichere amesema mapambano dhidi ya rushwa na uhalifu wa kifedha yanahitaji taasisi mbalimbali kufanya kazi kwa pamoja badala ya kila taasisi kutekeleza wajibu wake kwa kujitegemea.

Amesema ukaguzi wa Serikali haupaswi kuishia katika kubaini dosari baada ya fedha za umma kutumika, bali unapaswa pia kusaidia kutambua vihatarishi vinavyoweza kusababisha upotevu wa fedha, ubadhirifu na vitendo vya rushwa mapema.

No comments:

Post a Comment