Wednesday, July 12, 2017

WATU WAENDELEA KUTHIBITISHA MANENO YA KINABII WANAYOTAMKIWA NA NABII MKUU MH. DK GEORDAVIE.

                        Mtume Rose Abel akihudumu hii leo.{Picha na Deogratius Festo}
Watu mbalimbali wameendelea kuthibitisha maneno ya kinabii wanayotamkiwa Na Nabii Mkuu Mh. Dk GeorDavie kwani yameweza kuwatoa katika mateso mbalimbali yaliyokuwa yakiwasumbua kwa muda mrefu.

Hayo yamesemwa na Bi Happynnes Joseph mkazi wakati akizungumza na N.Y.U Radio ambapo amesema kuwa kwa kuamini nguvu ya mungu iliyopo katika madhabahu ya Ngurumo ya upako imeweza kumponya.  

Aidha Bi Happynnes amewataka watu wengine waendelee kuiamini nguvu iliyopo katika madhabahu ya Ngurumo ya upako kwani kupitia nguvu hiyo watu wengi wameponywa.

WAZIRI MPANGO AFUNGA KITUO CHA GBP KILICHOPO ENEO LA UWANJA WA NDEGE, DAR.





Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kuamuru kituo cha Mafuta cha GBP kifungwe hadi hapo kitakapo funga mashine maalumu za kutolea risiti baada ya kubainika hakitumii ipasanyo mashine za kieletroniki za kukusanyia kodi (EFD)

Dkt. Mpango amechukua hatua hiyo baada ya kujionea kituo hicho kikiwa na pampu nne za mafuta lakini kuna mashine moja pekee ya mkononi ya kutolea risiti jambo linasababisha wateja wao wengi kutopewa risiti na hivyo kuikosesha Serikali mapato yake na ni kinyume cha sheria za nchi.

“Sasa nawachukulia hatua ili liwe fundisho kwa wengine wote wanaouza mafuta nchini bila kufuata taratibu, na nitaanza na wewe, biashara yako isimame mpaka mashine zifungwe kwenye kituo chote na utekeleze mara moja,” alisema Dkt. Mpango

Katika ukaguzi wa Kituo cha Mafuta cha Puma, Dkt. Mpango amesifu utaratibu mzuri uliowekwa na kituo hicho kwa kufunga mashine maalumu za kutolea risiti zilizounganishwa na kila pampu za mafuta kitu ambacho ndicho Serikali inavitaka vituo vyote vya mafuta vitumie mfumo huo

“Kituo hiki kimezingatia sheria sheria kwa kufunga mashine kwa kuzingatia maelekezo ya Serikali na hapa tunauhakika wa kupata fedha za kuwatumikia wananchi, kinyume kabisa na kituo cha mafuta nilichokifungia, hapa ndio ningeomba Watanzania wanunue mafutaĆ¢€ aliongeza Dkt. Mpango.

Ameiagiza Mamlaka ya mapato Tanzania-TRA kufanya ukaguzi nchi nzima ili kubaini wamiliki wa vituo vya mafuta wanaokiuka maagizo ya Serikali yaliyowataka wafunge mashine hizo maalumu tangu mwaka uliopita.

Waziri wa Fedha na Mipango amewageukia wenye vyombo vya moto wanaonunua mafuta kwenye vituo vya mafuta kote nchini kudai risiti wanapopata huduma ya kuwekewa mafuta kwenye vituo hivyo ili kuokoa fedha za Serikali zinazoishia mikononi mwa wajanja wachache wanaokwepa kodi kwa makusudi na kuikosesha Serikali mapato yake.

Baadhi ya wananchi wamepongeza uamuzi wa Serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mipango wa kufanya ziara za kushitukiza kwenye vituo vya mafuta na kutaka hatua hiyo iwe endelevu kwa maafisa wengine wa Serikali ili kukomesha vitendo vya wenye vituo vya mafuta kukwepa kodi ya Serikali.

Katika siku yake ya kwanza ya ziara za namna hiyo, Julai 10 mwaka huu, Dkt. Mpango alikifungia kituo cha Mafuta cha Mawenzi kilichoko Kigamboni, Jijini Dar es Salaam baada ya kubaini kuwa kituo hicho kimefunga mashine maalumu za kutolea risiti za kielektroniki lakini hazitumiki na kuamuru kituo hicho kifungwe hadi kitakapo rekebisha kasoro hiyo na kuvionya vituo vya mafuta vya OilCom kufunga mashine za aina hiyo mara moja.

Tuesday, July 11, 2017

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA KATIKA IBADA YA CHUO CHA MANABII HII LEO.

 

Mchungaji mwanafunzi wa vijana Bi Suzan Nassary. 
 {Picha na Richard Shiyo}

Watu wametakiwa kumtegemea mungu katika kila jambo kwani kwa kufanya hivyo kuna faida kubwa ya kuwawezesha kuvuka katika maeneo mbalimbali.

Hayo yamesemwa na mchungaji mwanafunzi wa vijana Suzan Nasay alipokuwa akihubiri kwenye ibada ya chuo cha manabii iliyofanyika katika hema la kukutania kisongo Arusha.
 

   
Mchungaji Lidya Peter akihubiri leo hii. {Picha na Richard Shiyo}

Nae mchungaji Lidya peter amesema kuwa ni muhimu watu kuwa na mioyo ya shukrani pamoja na kutii ili waweze kufanikiwa katika maeneo mbalimbali.                      

Aidha watumishi wa mungu wanaotumika chini ya Nabii mkuu Mh Dk GeorDavie wamewafungua watu kutoka katika vifungo vya mateso.
           
                        Mwl. Mwanafunzi Annamesiah Masawe akihudumu leo hii.
                                             {picha na Richard Shiyo}
Ibada ya chuo cha manabii hufanyika kila siku za Jumanne na Alhamis ambapo watu kutoka sehemu mbalimbali ambapo watu uhudumiwa na watumishi wa mungu kwa ukaribu.

WATU WAKARIBISHWA KUHUDHURIA IBADA YA KATIKATI YA WIKI YA CHUO KIKUU CHA MANABII.




Kadinali wa tatu wa huduma ya Ngurumo Ya Upako Mchungaji Zimani Gervas amewaalika watu kutoka sehemu mbalimbali kuhudhuria ibada ya katikati ya wiki inayofanyika hii leo katika hema la kukutania kisongo Arusha.

Akizungumza na N.Y.U Radio amesema kuwa katika ibada ya katikati ya wiki watumishi wa mungu hufundisha neno la mungu kwa kifupi na mara baada ya neno la mungu hupita katikati ya watu kwa ajili ya kuwafungua watu kulingana na mahitaji yao.
Ameongeza kuwa ibada ya leo itakuwa ni ya baraka, hivyo watu watapokea miujiza, maongezeko na hatua mpya katika kila eneo.
Aidha amesema kuwa huduma ya ngurumo ya upako ipo kwa ajili ya watu wote kwani haichagui dini, kabila hivyo nguvu ya mungu ipo kwa ajili ya kuwahudumia watu wote.
 




Monday, July 10, 2017

MCHUNGAJI KIONGOZI WA N.Y.U DUNIANI MAMA ANNA DAVIE ATANGAZA UJIO WA NABII MKUU SIKU YA JUMAPILI TAR 16.07.2017



Mchungaji kiongozi wa huduma ya ngurumo ya upako duniani mama Anna Davie ametangaza ujio wa Nabii Mkuu Mh Dk Geor Davie jumapili ijayo katika ibada ya jiji  hemani kisongo.


 mama anna davie amesema hayo jana katika ibada ya jiji  kwenye hema kla kukutania kisongo arusha tanzania ambapo pia mama alisema kuwa nabii atakuwepo hivyo ni vyema watu wakaja kwa wingi kuja kupokea jambo jipya maishani.
katika ibada hiyo ya jiji balozi wa nabii mkuu tanzania mtume Sekela Ntondolo  alitoa maagizo kwa niaba ya nabii mkuu ,amabapo maagizo hayo ni kwajili ya kuwawezesha watu kupata upenyo na hatua mpya katika maisha yao.
katika ibada hiyo nabii william james wa huduma ya ngurumo ya upako  tawi la Dar es Salaam  la city centre alifundisha somo lenye kichwa kisemacho nyumbani ambapo amewataka watu kupokea maonyo wakiwa nyumbani kwani ndiyo sehemu ya kwanza ya kupata malezi yatakayowasaidia maishani.
watu walihudhuria ibada hiyo pia wamefurahishwa na ibada hiyo ,ila pia juu ya ujio wa nabii mkuu tz jumapili ijayo na hivyo wamewataka watu waweze kuhudhuria ibada hiyo bila kukosa wakiwa na sadaka maalumju.



JPM: TUJIFUNZE KUTUMIA FEDHA VIZURI ZA SERIKALI ASITOKEE MCHWA KULA PESA ZA SERIKALI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kote nchini na kuwataka kuwa na nidhamu ya pesa na kutumia fedha za serikali vizuri.

Rais Magufuli amesema hayo leo wilayani  Chato mkoani Geita alipokuwa akihutubia wananchi katika makabidhiano ya nyumba 50 zilizojengwa na taasisi ya Benjamin Mkapa, ambapo mbali ya kushukuru kwa msaada huo Rais Magufuli alizungumzia juu ya tabia ya baadhi ya viongozi wa serikali kuiba fedha za wananchi na kutumia katika mambo yao wenyewe nje ya malengo ya serikali.

"Hapa penyewe Chato kuna fedha zaidi ya bilioni moja za pembejeo zimeliwa na viongozi, hivyo natoa wito kwa viongozi wote wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kote nchini kuwa na nidhamu na fedha za serikali, tujifunze kutumia fedha vizuri  za serikali asitokee mchwa huko kula pesa za serikali. Maana hili lililotokea hapa Chato najua limetokea sehemu nyingi na hivyo saizi tunaanza kufanya ukaguzi kila sehemu" alisema Rais Magufuli

Mbali na hilo Rais Magufuli aliwataka wananchi wa hali ya chini kuwa na amani kwani katika kipindi chote ambacho yeye atakuwa madarakani hataki kuona wala kusikia wananchi wa hali ya chini wakinyanyaswa sababu na yeye ametokea katika maisha hayo hivyo anatambua jinsi wanavyopata shida watu wa kipato cha chini.

"Serikali haiwezi kufanya biashara na masikini, inawaacha matajiri inawasumbua masikini, mimi nimekuwa katika maisha ya shida nimechunga ng'ombe, nimeuza maziwa kwa hiyo najua maisha ni nini. Najua Tanzania watu wengi wanaishi maisha ya chini na katika kipindi changu sitaki kuona watu wa hali ya chini wanapata shida, wanapata taabu ndiyo maana tunajitahidi kuhangaika kuleta maendeleo ili wanufaike na wao" alisisitiza Magufuli

Rais Magufuli akuziacha taasisi ambazo zimekuwa zikitetea wanafunzi kupata mimba na kusema yeye taasisi hizo hazipendi na ameziwekea kizingiti kuwa ikiwezekana zisipewe msaada bali taasisi zinazofanya mambo ya kimaendeleo kama taasisi ya Mkapa Foundation ndiyo zinatakiwa kupewa msaada sana kwa kuwa zinarudi kuleta maendeleo kwa wananchi.