Sunday, November 17, 2019

#NENO LA WIKI HII KINABII LATANGAZWA/NABII MKUU KUWEPO TENA JUMAPILI IJAYO/WAGENI HAWA KUHUDHURIA

NABII MKUU TANZANIA MH DKT GEORDAVIE AMETANGAZA KUWA HII NI WIKI YA MAWAZO YAKO KUPATA KIBALI,

NABII MKUU AMETANGAZA NENO HILO HII LEO KATIKA IBADA YA CHUO KIKUU CHA MANABII HEMANI KISONGO ARUSHA AMBAPO ILIKUWA NI IBADA YA KUPATANISHWA NA MADHABAHU.

NA NABII MKUU AMESEMA HIVI
"LAKINI LEO NIMEKUAMBIA WIKI YA MAWAZO YAKO KUPATA NINI?KIBALI, SASA KAA NIKUELEZE MAWAZO YAKO YATAKAVYOPATA KIBALI.
"MUNGU HUMPA BARAKA MTU MWENYE AKILI TIMAMU,
AMEN.
"SEMA NINA AKILI TIMAMU, NIPO TAYARI KUPOKEA BARAKA YANGU"
"KATIKA ZABURI 19 :14 ,BIBLIA INASEMAJE, MANENO YA KINYWA CHAKO NA MAWAZO , YA MOYO WANGU YAPATE KIBALI MBELE ZAKO EE BWANA MWAMBA WANGU NA MWOKOZI WANGU ,"
NA NDIO MAANA NIKAKWAMBIA NI WIKI YA MAWAZO YAKO KUPATA KIBALI"
NABII MKUU MH DKT GEORDAVIE AMEENDELEA KUSEMA KUWA "UTAANDIKA MAWAZO SITA YAANI MAMBO SITA YANAYOTOKA KWENYE MAWAZO YAKO KWA SABABU NI WIKI SAHIHI YA MAWAZO YAKO KUPATA KIBALI,KWA MAANA YA KWAMBA HAYO MAWAZO SITA AU MAMBO SITA NI KATIKA NDOTO ZAKO ,MAMBO ULIYOKUSUDIA KUYAONA YANATOKEA KATIKA MAISHA YAKO UTAYAANDIKA WIKI HII ,MATATU JUMANNE NA MATATU ALHAMISI,UTAFUATISHA WATU WATAKAO KUWA WAKIONGEA REDIONI KUANZIA SAA TATU MPAKA SAA NNE USIKU UTAKAPOTOA SADAKA YAKO MAALUMU KUANZIA SH 5000 KAMA UNA UWEZO HUO AU 10,000 KAMA UNAUWEZO HUO UNAJUWA UWEZI KUPOKEA KITU KIKUBWA BILA KUWEKEZA KATIKA KITU HICHO,NA HIYO ITAKUWA NI SADAKA YAKO MAALUMU UTAKAYOANDIKA KATIKA NAMBA YA KUINUA MIKONO "
"NA NDIO NAKUUNGANISHA NA FREQUENCY ZA KUPOKEA YALE UTAKAYOANDIKA"
MBALI NA HAYO NABII MKUU AMETANGAZA KUWEPO TENA JUMAPILI IJAYO YA TAREHE 24/11/219 AMBAPO ITAKUWA NI SIKU YAKUPANDISHWA NGAZI INGINE KWA NJIA YA UNABII,HUKU WAGENI KUTOKA TAWI LA HUDUMA YA NGURUMO YA UPAKO MAREKANI WANATARAJIWA KUWEPO PIA.
NABII MKUU AMESEMA "NA WIKI IJAYO NITAKUWEPO HAPA KWA HIYO NINATAKA UMWALIKE NA MWEZAKO,UMWALIKE NA MWEZAKO,ITAKUWA NI SIKU YA KUPANDISHWA NGAZI NYINGINE KWA NJIA YA UNABII,NA MAAGIZO NI YALE UTAKUJA UMEFUNGA NA SADAKA MALUMU YA SH 20,000 KWAAJILI YA KUPANDISHWA NGAZI NYINGINE"
HATA HIVYO NABII MKUU ALIFANYA HUDUMA YA UNABII NA KUWABARIKI VIJANA WOTE WALIOSHIRIKI IBADA HIYO,NA ALIWATAMKIA MATAMKO MAALUMU.
**********MWISHO*********

No comments:

Post a Comment