Thursday, March 28, 2019

AJENGEWA NYUMBA, WENGINE WASAPOTIWA FEDHA..

Kanisa dogo la mkoani Kilimanjaro lililopatiwa msaada na Nabii Mkuu.

Nyumba mpya anayojengewa Bi. Nawasa ikiwa inaendelea na ujenzi.
Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametoa msaada wa jumla ya sh. 2,300,000 (milioni mbili na laki tatu), kwa watu watatu tofauti huku mwingine akipata neema ya kujengewa nyumba.
Hayo yamejiri wiki hii baada ya Nabii Mkuu kuguswa kuwasaidia watu wawili tofauti mtaji wa sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kila mmoja kwa ajili ya kuwawezesha kupata mtaji wa kuanzisha biashara.
Kwa upande mwingine Mchungaji mmoja wa kanisa dogo mkoani Kilimanjaro (jina lake na la kanisa linahifadhiwa) amebarikiwa sh. 300,000 (laki tatu) mara baada ya Nabii Mkuu kuliona kanisa hilo la mbao (kama linavyoonekana pichani) wakati akipita na msafara wake na kuwakuta katika ibada yao ambapo aliguswa kushuka na kuwasapoti kifedha na kisha kuendelea na safari yake.
Mchungaji huyo pamoja na waumini wake wasiozidi kumi (10) wakizungumza mara baada ya kupokea baraka hiyo ya kifedha walionyesha furaha yao na kutoa shukurani zao za dhati kwa Nabii Mkuu kutokana na msaada huo.
Wakati huohuo mwanamke mmoja muumini wa huduma ya Ngurumo Ya Upako anayefahamika kwa jina la Nawasa Saibulu, amepata neema ya kipekee ya kujengewa nyumba na Nabii Mkuu (kama inavyoonekana pichani ikiwa inaendelea na ujenzi) baada ya nyumba ya awali aliyokuwa akiishi iliyokuwa ya udongo kuharibika na kuwa na tatizo la kuingiza maji kipindi cha mvua.
Mwanamke huyo ni miongoni mwa watu waliopata neema hiyo ya kuboreshewa makazi yao kwa mwaka huu wa 2019.
Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie amekuwa na kawaida ya kutoa misaada mbalimbali ya kifedha ambapo tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2019 ametumia zaidi ya sh. 40,000,000 (milioni arobaini) katika kugusa mahitaji mbalimbali ya watu kutoka sehemu tofauti tofauti duniani.


NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio

Wednesday, March 27, 2019

WABARIKIWA FEDHA KWAAJILI YA KUKUZA BIASHARA ZAO..Neema ya kifedha imewatembelea baadhi ya watu waliokuwa na mahitaji ya fedha kwaajili ya kukuza biashara zao pamoja na kulipa madeni, ambapo Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie aliwapatia fedha taslimu kwaajili ya kukidhi mahitaji yao.
Ni siku ya jumapili katika Ibada ya jiji, iliyofanyika katika katika hema la kukutania Ngurumo Ya Upako.. Kisongo, Arusha ambapo jumla ya 1,200,000 (milioni moja na laki mbili) ilitolewa nae Nabii Mkuu kwaajili ya kuwa-support kwenye shughuli zao waweze kujikimu kimaisha.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti watu hao wameelezea ugumu waliokuwa wakiupata kiuchumi na wepesi waliouona mara baada ya kubarikiwa kifedha nae Nabii Mkuu na kuahidi kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha wanaitendea haki fedha waliyopewa na Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie.
Aidha siku ya jumapili katika Ibada ya Chuo Kikuu Cha Manabii ilikuwa ibada ya "Kupatiwa uelekeo mpya na sahihi maishani" ambapo Nabii Mkuu alifanya Huduma ya Unabii wa mtu mmoja mmoja wa kupita katikati ya maelfu ya watu waliofika siku ya jana na kuwahudumia kila mmoja kwa nafasi yake.
Akizungumza Nabii Mkuu alisema kuwa watu wengi wanateseka maishani kwa sababu ya uelekeo mbaya/ usiokuwa sahihi waliokuwa nao ambao huwapelekea kuteseka kwa maumivu na vifungo mbalimbali vya nguvu za giza, ambapo Nabii Mkuu aliwafungua na kuwatamkia matamko mbalimbali ya kuwapatia uelekeo mpya.
Wakati huo huo Nabii Mkuu ametangaza kuwepo tena jumapili ya tarehe 31/3/019 itakayokuwa ibada kufidiwa muda uliopotea.

NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio

Tuesday, February 19, 2019

WAPEWA PESA ZA MITAJI MIDOGO...!!


Jumla ya sh. Milioni moja, laki tisa na elfu hamsini (1,950,000) zimetolewa na Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie kwa watu takribani kumi (10) wenye uhitaji wa aina mbalimbali waliojitokeza.
Ni katika ibada ya Chuo Kikuu Cha Manabii iliyofanyika katika hema la kukutania Ngurumo Ya Upako, ambapo Nabii Mkuu aliwataka watu wenye uhitaji wa pesa za kujikimu kujitokeza ambapo watu hao walijitokeza na kuweza kupata Neema hiyo ya kusaidiwa na Nabii Mkuu.
Pia watu wengine tofauti tofauti kwa nyakati tofauti wameweza kufikiwa na neema ya kusaidiwa kifedha na Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ambapo amekuwa akituma pesa kwa kadiri jinsi Roho Wa Mungu amekuwa akimuongoza kuwasaidia watu hao ambao wamekuwa wakimuelezea uhitaji wao pamoja na hali ngumu wanazopitia kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kupitia namba ya kunyanyua mikono ya Nabii.
Aidha Nabii Mkuu anatarajia kuwepo siku ya ijumaa katika hema la kukutania Ngurumo Ya Upako, Kisongo, Arusha ambapo itakuwa ni siku ya International Partners (IP) siku ambayo ni maalum kwa wana-International Partners kuwasilisha michango yao kwaajili ya ku-support GeorDavie Tv mikononi mwa Nabii Mkuu.

NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio

Monday, February 4, 2019

ALIPIWA DENI, KODI NA MTAJI..

"Mungu amenikumbuka, ameniona na amenifuta machozi" ni kauli ambayo ilitolewa na mwanamama aliyesaidiwa na Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie baada ya kulipiwa kodi ya nyumba ya mwaka mzima pamoja na miezi mingine minne aliyokuwa akidaiwa ambapo pia aliongezewa mtaji wa biashara yake.
Mwanamama huyo anayefanya biashara ndogo ndogo alifika akilia mbele ya Nabii Mkuu ambapo alisema kuwa amekimbiwa na mume na kuachiwa watoto wanne, wakiwa wanaishi katika chumba kimoja ambacho alikuwa akidaiwa kodi ya miezi minne pamoja na watoto wake.
Baada ya kujieleza Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie alitoa pesa taslimu na kumkabidhi ili aweze kulipa kodi hiyo aliyokuwa akidaiwa pamoja na kumuongezea nyingine kwa ajili ya mwaka mzima ambapo alimuongezea mtaji wake ili aweze kujikimu na maisha.
Akizungumzia hilo Nabii Mkuu amesema kuwa Serikali Tukufu Ya Ufalme Wa Mungu imeamua kugusa matatizo ya kifedha waliyonayo watu wake ili kuhakikisha shida zinawapungukia na hatimaye kuisha kabisa.
Hayo yamejiri siku ya jana katika ibada ya Chuo Kikuu Cha Manabii, Ngurumo Ya Upako, ambapo ilikuwa ni ibada ya "Kufuta kumbukumbu zote mbaya maishani" ikiongozwa nae Nabii Mkuu.
Akizungumza katika ibada hiyo Nabii Mkuu alisema kumbukumbu mbaya hufanya watu wasipige hatua katika maisha, waishi wakiwa na huzuni pamoja na chuki ambapo alitamka matamko ya Kinabii kwaajili ya kuwatenganisha watu na hali hiyo.
Wakati huo huo Nabii Mkuu anatarajia kuwepo katika kipindi cha "Q and A AKILI KUBWA" siku ya leo kuanzia saa mbili na nusu za usiku, kipindi kitakachoruka kwa kupitia 99.3 N.Y.U Radio pamoja na GeorDavie Tv ambapo jumla ya 2,000,000 (milioni mbili) zitatolewa kwa washindi watakaoweza kujibu maswali kwa ufasaha kabisa.

NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio.

Sunday, February 3, 2019

ZAIDI YA MILIONI 14 YATOLEWA KWA JAMII- JANUARY..Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametoa zaidi ya sh. 14,490,000 (Milioni kumi na nne, laki nne na elfu tisini), kwa mwezi wa January kama zawadi na misaada kwa watu mbalimbali.
Fedha hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti tofauti kwa kupitia vipindi mbalimbali vilivyokuwa vikiruka kupitia 99.3 N.Y.U FM pamoja na GEORDAVIE TV lakini wengine wakiweza kujipatia zawadi zao kwa kupitia ibada za Chuo Kikuu Cha Manabii.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya watu walioweza kujishindia zawadi hizo, wamemshukuru Nabii Mkuu kwa zawadi hizo huku wakieleza pia jinsi ambavyo fedha hizo zimeweza kuwasaidia katika maeneo mbalimbali maishani mwao ikiwa ni pamoja na kutatua matatizo ambayo walikuwa nayo.
Katika mwaka huu wa 2019 ambao ni "Mwaka wa kujenga uwezo" Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie, amesema kuwa hizi ni Zama Mpya ambapo Serikali tukufu ya Ufalme wa Mungu inawagusa watu wenye mahitaji kwa njia ya tofauti ambayo ni ya kuwasaidia kifedha na huu ukiwa muendelezo wa zoezi hilo lililoanza mwishoni mwa mwaka jana na bado likiwa endelevu.

NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio

Friday, January 25, 2019

VITUO VYA WATOTO YATIMA VYAPOKEA MSAADA WA CHAKULA.
    Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametoa misaada ya vyakula vyenye thamani ya sh. 3,120,000 (milioni tatu laki moja na elfu ishirini) kwa vituo viwili vya watoto yatima siku ya leo.
   Misaada hiyo imekabidhiwa asubuhi ya leo kwa niaba ya Nabii Mkuu nae Mngojezi wa Nabii Mkuu, Bw. Abiud Luila kwa wasimamizi wa vituo vya Faraja Orphanage center, Bw. Faraja, pamoja na kwa msimamizi wa kituo cha Christian Woman Orphanage Care anayeitwa Mchungaji Zakia Hatib.
   Vitu vilivyotolewa ni pamoja na mchele kg. 600 wenye thamani ya sh. 1,320,000 (milioni moja, laki tatu na elfu ishirini), mafuta ya kupikia lita 300 yenye thamani ya sh. 1,200,000 (milioni moja na laki mbili) pamoja na sukari kg. 240 yenye thamani ya sh. 600,000 (laki sita).
   Wakizungumza baada ya kupokea misaada, wasimamizi wa vituo hivyo wametoa shukurani zao za dhati kwa Nabii Mkuu kwa upendo wake pamoja na moyo wa kusaidia alionao kwa watu wote bila kujali dhehebu, dini wala kabila.
   Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie amekuwa na kawaida ya kutoa misaada mbalimbali katika vituo vya watoto yatima kila mwanzo wa mwaka ambapo zoezi hilo litaendelea kwa vituo vingine.

NB: Usisahau kudownload application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama  GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio
Pichani ni Mngojezi wa Nabii Mkuu, Bw. Abiud Luila (kushoto) akikabidhi misaada kwa niaba ya Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie,  kwa msimamizi wa kituo cha Faraja Orphanage.
Baadhi ya vitu vilivyotolewa kama misaada katika vituo vya watoto yatıma.

Baadhi ya vitu vilivyotolewa katika  vituo vya watoto yatima.

Baadhi ya vyakula vilivyotolewa kwa watoto yatima.

Katika picha ni Mngojezi wa Nabii Mkuu, Bw. Abiud Luila (kushoto) katika picha ya pamoja na Msimamizi wa kituo cha Christian Woman Orphanage Care, wakati akimkabidhi misaada kwa niaba ya Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie.

Tuesday, January 22, 2019

ATOA ZAWADI YA PIKIPIKI NA PESA KEM KEM KAMA ZAWADI KWA WATU WALIOWEZA KUJIBU MASWALI!


Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie amezidi kubariki jamii kwa kumwaga pesa ikiwa ni mara baada ya kutoa zawadi ya pikipiki pamoja na pesa taslim, zaidi ya shilingi milioni moja kama zawadi.

Nabii Mkuu alitoa zawadi ya Pikipiki yenye thamani ya shilingi Milioni mbili na laki nne (2,400,000) kwa Ndugu. Tito Paul pamoja na zawadi ya pesa alizojishindia kwa kujibu maswali aliyomuuliza kwa ufasaha kabisa.
Kwa upande wake Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie akizungumzia hilo amewataka watu kuchangamkia nafasi ya kujibu maswali hayo kwani kwa kufanya hivyo watajiongezea nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali kama magari, nyumba, pikipiki na pesa za mtaji, ada na za kujikimu katika mahitaji mengine.
Akielezea mgawanyiko wa maswali yanayoulizwa katika vipindi hivyo Nabii Mkuu amesema kuwa maswali hayo yamegawanyika katika sehemu tatu (3).. 60% yakiwa yanahusu huduma, 20% N.Y.U Radio na 20% nyingine yakiwa yanahusu GeorDavie Tv ambapo watu wametakiwa kufuatilia vipindi kwa makini pamoja na kuhudhuria ibada katika Hema la Kukutania Ngurumo Ya Upako ili kupata uelewa zaidi wa kuweza kujieleza ili waweze kushinda zawadi hizo.
Akifafanua zaidi Nabii Mkuu amesema kuwa haya ni majira mapya ambayo Serikali Tukufu Ya Ufalme Wa Mungu inawabariki watu wake kwa njia ya tofauti ambapo amesema kuwa zoezi hilo bado linaendelea.
Tangu kuanza kwa mwaka huu Nabii Mkuu ametoa zaidi ya shilingi milioni nane (8) kwa jamii, ambapo zawadi hizo watu wamekuwa wakijishindia kwa njia ya kujibu maswali katika vipindi mbalimbali vinavyoruka kupitia 99.3 N.Y.U RADIO pamoja na GEORDAVIE TV.
Katika muendelezo wa utoaji wa zawadi hizo Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametangaza kuwepo tena katika kipindi cha "Q & A AKILI KUBWA" kitakachoruka Live kwa njia ya 99.3 N.Y.U RADIO pamoja na GEORDAVIE TV jumatano ya week hii, kuanzia majira ya saa mbili na nusu usiku, ambapo atakuwa akiuliza maswali na kutoa zawadi ya pesa kwa washindi watakaojibu vizuri.
Aidha Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ameitangaza week hii kuwa ni week ya kung'oa kila pando la adui na mabaya yote na kuongeza kuwa week hii Roho Wa Mungu atadumu kung'oa kila pando la adui lenye lengo la kudhoofisha watu.
NB: Usisahau kudownload application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio

Tuesday, January 15, 2019

NABII MKUU MHE. DR. GEORDAVIE ATANGAZA WIKI YA USHINDI KATIKA MAENEO YOTE MAISHANI.
 KUTOKA IKULU YA NABII MKUU TANZANIA..

    Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametangaza kuwa hii ni wiki ya kuwa washindi katika maeneo yote maishani.
    Ameyasema hayo wakati akiongoza ibada ya chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika hema la kukutania, Ngurumo Ya Upako, Kisongo, Arusha.
   Katika ibada hiyo ambayo pia ilikuwa ni ibada ya Silver Partners, Nabii Mkuu alitamka baraka mbalimbali za Kinabii kwa wana-Partners wote ikiwemo baraka ya kushika pesa na kuheshimika.
   Aidha Nabii Mkuu alifundisha umuhimu wa kuwa mwana-Partners na faida zake huku akiwasisitizia watu wote kusapoti kazi ya Mungu kwa nguvu kwa kuna baraka ya kipekee wataipata kwa kufanya hivyo na kuwakumbusha kuwa ili kazi ya Mungu iwe nzuri na ithaminiwe ni lazima igharamikiwe ambapo alitoa nukuu isemayo "Cha gharama kina thamani kama hakina gharama hakina thamani" akimaanisha kuwa kitu chochote chenye thamani lazima kiwe cha gharama hakiwezi kuwa bure ikiwemo Nguvu Ya Mungu.
   Wakati huohuo Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametangaza kuwepo katika kipindi cha Maswali Na Majibu  kitakachoruka LIVE kwa njia ya Radio,  99.3  N.Y.U FM pamoja na GEORDAVIE TV siku ya jumatano ambapo kwa siku hiyo yeye ndiye atakayeuliza maswali kwa wasikilizaji na watazamaji na kisha kutoa zawadi ya pesa taslimu kwa wale watakaopatia kwa kujibu maswali hayo vizuri. 


          NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama  GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio.

Tuesday, January 8, 2019

JE UNAFAHAMU KUWA MHE. DR. GEORDAVIE KATIKA MWAKA 2018 PEKEE AMETUMIA ZAIDI YA SH. MILIONI 143 KATIKA KUSAIDIA JAMII???


   Amekuwa akitambulika kama Mtumishi wa Mungu mtoaji zaidi Nabii wa Equator, Nabii Mkuu wa karne ya 21, si mwingine ni Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie kutoka Arusha, Tanzania.
  Na siku ya leo tunakuletea kwa uchache baadhi ya matukio ya utoaji aliyoweza kuyafanya kwa mwaka wa 2018 yaliyopelekea Nabii Mkuu ambaye amekuwa msaada na kipenzi cha wengi kutajwa kama Mtumishi Wa Mungu mtoaji zaidi.
  Katika ku-support Watumishi Wa Mungu kutoka katika makanisa mengine tofauti na Ngurumo Ya Upako yaliyo ndani na nje ya Tanzania, Nabii Mkuu ametumia zaidi ya Sh. Milioni 30 katika kuhakikisha anatoa misaada katika huduma hizo ambapo kwa asilimia kubwa zilikuwa haziridhishi kiuchumi (hazijamudu kujitegemea kiuchumi), Nabii Mkuu aliweza kuwasaidia ili kuhakikisha watumishi wanaweza kukidhi mahitaji yao lakini pia ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kujenga makanisa yao ili yawe katika hali ya kuridhisha.
  Katika upande mwingine wa kijamii, Nabii Mkuu amekuwa na kawaida ya kupeleka misaada sehemu mbali ikiwa ni pamoja na katika vituo vya watoto yatima ambapo kwa mwaka 2018 Nabii Mkuu amepeleka katika vituo vitatu tofauti hapa Tanzania.
   Mbali na hayo pia Nabii Mkuu ametoa misaada mingine ikiwemo kuwalipia ada wanafunzi wa ngazi mbalimbali mpaka chuo kikuu waliokwama kutokana na kukosekana kwa kipato ili kuwawezesha kuendelea na masomo yao.
  Aidha katika kusaidia watu pia Nabii Mkuu ametumia zaidi ya Milioni 20 katika kusaidia watu mbalimbali wenye mahitaji, ikiwemo wenye uhitaji wa mitaji lakini pia wenye biashara ndogo ndogo katika kuhakikisha wanaweza kuwa na kipato cha kujikimu kimaisha.
  Lakini pia katika upande mwingine Nabii Mkuu amekuwa akiwa-support watu wenye vipaji kwa namna mbalimbali ambapo baadhi ya waliopata neema hiyo ni pamoja na vijana wawili walionunuliwa ngoma na mwingine spika ,kila mmoja kwa wakati wake pamoja na waimbaji wa nyimbo za injili kutoka sehemu mbalimbali.
  Hakuishia hapo katika kusaidia tu, Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie amekuwa akitoa zawadi mbalimbali kwa watu ambapo kwa mwaka wa 2018 ametoa zawadi ya magari nane (8) kwa watu tofauti tofauti wa ndani na nje ya nchi kwa mwaka huo yenye thamani ya jumla milioni 88.
  Aidha katika msimu wa sikukuu mpaka sasa Nabii Mkuu ametoa zawadi kwa njia ya pesa taslimu za zaidi ya sh. Milioni 5 kwa watu mbalimbali ambao walijishindia kwa njia ya kupiga simu kwenye vipindi vilivyokuwa vikiruka kupitia 99.3 N.Y.U FM Radio pamoja na GeorDavie Tv (zoezi hilo linaendelea mpaka sasa) na wengine wakijishindia kupitia mitandao ya kijamii.
  Akizungumzia utoaji huo Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie amesema haya "hiyo ni njia ya Ufalme Wa Mungu kuwabariki watu wake kwakuwa nao wamekuwa wakitoa kwa Ufalme Wa Mungu hivyo sasa ni wakati wao kubarikiwa pia" mwisho wa kunukuu.
         NB: Usisahau kudownload application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio.

Tuesday, December 25, 2018

NABII MKUU MHE. DR. GEORDAVIE AMEWATAKA WATU KUTOKUANGALIA MAZINGIRA YANASEMA NINI BALI WAANGALIE KUSUDI LA MUNGU KATIKA MAISHA YAO.

   Jumapili ya tarehe 23.12.018 Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie aliongoza ibada ya jiji katika Chuo Kikuu Cha Manabii Ngurumo Ya Upako Arusha, ambapo ilikuwa ni ibada ya Christmas ya kudhihirisha kusudi la Mungu maishani.

   Akifundisha somo lenye kichwa kisemacho "Usiangalie mazingira bali kusudi la Mungu" Nabii Mkuu amesema kuwa kuna wakati mazingira yanaweza kueleza kitu kingine lakini pia Mungu akawa na kusudi maishani mwako ambapo alimtolea mfano Yesu Kristo na kusema kuwa kuzaliwa kwake katika hori la ng'ombe haikuwa sababu ya kusudi alilokuwa nalo kupotea.
   Aidha Nabii Mkuu amesema kuwa katika maisha kuna vitu vitatu.. Mazingira, Wakati na Kusudi na kuongeza kwamba "Mazingira hukabiliwa na wakati" ikiwa siyo wakati wa Mungu huwezi kulazimisha na pia ikiwa ni wakati wa Mungu huwezi kuuzuia.

   Mbali na hayo Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeoDavie alifungua watu mbalimbali waliofika wakiwa na vifungo vya nguvu za giza, na pia kutamka maneno ya baraka kwa watu wote ili wazidi kuinuka, kubarikiwa, kung'aa na kufanikiwa.

   Pia Nabii Mkuu ametangaza kuwepo tena katika katika hema la kukutania Ngurumo Ya Upako siku ya jumatano ya tarehe 26.12.018 ambapo itakuwa ni ibada ya hitimisho la Siku kuu ya kukusanya (SKYK) ambapo watu wote wametakiwa kufika wakiwa wamefunga pamoja na bajeti zao za mwaka 2019.


    NB: Usisahau ku-download application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama  GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio.

Monday, December 10, 2018

NABII MKUU MHE. DR. GEORDAVIE AONGOZA IBADA YA MWISHO KWA SILVER PARTNERS.KUTOKA KATIKA IBADA YA JIJI, CHUO KIKUU CHA MANABII, ILIYOFANYIKA KATIKA HEMA LA KUKUTANIA NGURUMO YA UPAKO, KISONGO, ARUSHA..
Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie aliongoza ibada ya chuo kikuu cha manabii siku ya jana ambapo ilikuwa ni ibada ya Silver Partners ya mwisho kwa mwaka huu wa 2018, ambapo aliweza kutamka baraka mbalimbali kwa wana-Silver Partners wote.