Thursday, November 2, 2023

NABII MKUU MHE. DKT. GEORDAVIE AWAFUTIA MAELFU YA WATU MAPIGO MATATU ADUI ALIYOKUSUDIA KUWADHURU

Nabii Mkuu Mhe. Dkt. GeorDavie Balozi wa amani amewafutia maelfu ya watu mapigo matatu ambayo adui alikusudia kuwadhuru watu wa Mungu. 

Nabii Mkuu amefuta mapigo hayo ambayo ni ajali, kifo cha ghafla na janga la uharibifu kupitia kipindi maalum kilichorushwa live kupitia N.Y.U Radio jumatano usiku ambapo Mungu alimpa dhamana ya kufutia watu mapigo hayo.

Akitamka matamko ya kufuta mapigo hayo Nabii Mkuu amesema kuwa Mungu amekukusudia kupokea uzima na uhai na watu wamepokea amani, kuwa salama na kuwa vyema.

Akizungumza katika kipindi hicho Nabii Mkuu amesema kuwa jambo kama hilo haliwezekani kwa maombi bali linamuhitaji Nabii Mkuu ili kutoa maelekezo.

Aidha watu walipata nafasi ya kutuma sadaka zao maalum za kuepuka mapigo yote matatu ya adui sawasawa na maagizo ya Nabii Mkuu.

Na Beatrice Maina, N.Y.U ARUSHA.



No comments:

Post a Comment