Monday, November 27, 2023

NABII MKUU MHE. DKT. GEORDAVIE AISHUKURU SERIKALI KWA KUMPA BARABARA.

Nabii Mkuu Mhe Dkt.GeorDavie ameishukuru serikali kwa kutambua mchango wake katika jamii na kumpa heshima ya kuandika jina lake na huduma yake kwenye barabara mbili hapa jijini Arusha ambapo kuna barabara ya GeorDavie Road na Ngurumo ya Upako Road.

Akizungumza Nabii Mkuu amesema kuwa ataendelea kusaidia wananchi na kwamba furaha yake ni kusaidia watu huku akisema amefanya mambo mengi mema kwa watu na hakutarajia siku moja atapewa heshima kubwa kama hii ya kupewa Barabara ambazo zitakuwa ni historia hata kwa vizazi vijavyo.

Aidha kwa hapa nchini hatujaona barabara nyingine yenye jina la Mtumishi wa Mungu na Nabii Mkuu Mhe Dkt.GeorDavie amekuwa Mtumishi wa Mungu wa kwanza kupewa barabara zenye jina na huduma yake ambapo GeorDavie Road ipo barabara ya kuelekea Ikulu ya Nabii Mkuu.

Kuna Barabara nyingine kama Nyerere, Ally Hassan Mwinyi, Kawawa Road, Sokoine Road na Sasa tuna Barabara ya GeorDavie na Ngurumo ya Upako Road ambapo zinapatikana Barabara ya Dodoma Arusha.



No comments:

Post a Comment