HABARI ZA HUDUMA

Kadinali wa pili wa huduma ya ngurumo ya upako mchungaji Elizabeth Hamphrey amewakumbusha watu wote kuhudhuria ibada ya Baraka ya chuo cha manabii itakayofanyika siku ya kesho katika hema la kukutania kuanzia saa sita kamili mchana.
Akizungumza na N.Y.U Radio  Mchungaji Elizabeth Humphrey amesema kuwa ni vyema kila mmoja kufika mbele za bwana ili kufundiswa neno la Mungu ikiwa ni
pamoja na  kupokea nguvu ya Mungu kutoka kwa watumishi wa mungu wanaotumika chini ya Nabii mkuu mh. Dk. GeorDavie.

Ameongeza kuwa watu kuhudhuria  ibada hiyo wataendelea kujazwa neno la mungu ikiwa ni pamoja na kuchota Baraka ambazo Nabii mkuu amekuwa akiziachilia katika madhabahu.
Habari Na Ngurumo ya Upako.



Alhamis,July27,2017.
WATU WAALIKWA KUHUDHURIA IBADA YA CHUO CHA MANABII HII LEO.
Huduma Ya Ngurumo Ya Upako Duniani siku ya leo kutafanyika ibada ya Chuo Cha Manabii inayoanza kuanzia smuda wa saa sita mchana {12:00} ambapo watu mbalimbali wamealikwa kuhudhuria ibada hiyo.

Akizungumza na N.Y.U Radio Kadinali wa tatu wa Huduma ya ngurumo ya upako Mchungaji Zimani Gervas amesema kuwa ni vyema watu wakahudhuria ibada hiyo kwani watu mbalimbali wameponywa na kuwa huru ikiwa ni pamoja na
kujifunza namna ya kuutunza muujiza.
Aidha Huduma ya nurumo ya upako ibada ya katikati ya wiki ni kila siku za Alhamis na Jumanne ambapo watu kuoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Arusha hufika katika hema la kukutania kwa ajili ya kupokea uponyaji.
                                                                      Habari Na Ngurumo ya Upako.


Jumatano,July19,2017

WATUMISHI WA MUNGU KUTOKA MAKANISA MBALIMBALI WAITIKIA WITO ULIOTOLEWA NA MH NABII DK. GEORDAVIE.
 Watumishi wa mungu kutoka maeneo mbalimbali wameitikia wito uliotolewa na Nabii Mkuu Mh Dk GeorDavie  wa kushiriki katika ibada ya chuo kikuu cha manabii itakayofanyika katika hema la kukutania ngurumo ya upako kisongo siku ya jumapili.














Wakizungumza kwa njia ya simu katika kipindi cha Radio Chuo kinachorushwa na N.Y.U Radio watumishi  ambao ni Mtume Elisifa Kefas na Nabii Lightnes Mollel wameonyesha kuupokea wito huo.
 









Wito  huo ulitolewa na Nabii Mkuu Mh Dk GeorDavie  siku ya jumapili  katika ibada ya jiji iliyofanyika katika hema 
la kukutania kisongo Arusha.

Habari Na Ngurumo ya Upako.

WAMAMA WATAKIWA KUJIANDAA VYEMA KUPOKEA NGUVU YA MUNGU SIKU JUMAPILI YA TAR.23
Wamama wametakiwa kujiandaa vyema na kuweka maandilizi tayari ili kuweza kupokea nguvu ya mungu na Baraka za mungu zitakazo achiliwa siku ya jumapili katika ibada ya chuo kikuu cha manabii.

Hayo yamesemwa na wamama siku ya jana wakati wakizungumza katika kipindi cha wamama na majukumu kinachorushwa na N.Y.U Radio ambapo wamama hao wamewataka wamama wenzao kuja na waache visingizio vya kukabiliwa na kazi   .
Aidha bi Anna Numi ambaye ni afisa masoko wa N.Y.U Radio amesema
maandalizi ni  jambo la kuzingatia kwa sababu bila maandalizi huwezi kufanya vitu na kufanikiwa.
Kwa upande wake Mchungaji Anna Pita Salanje wa huduma ya ngurumo ya upako amesema kukiwa na kiongozi mzuri lazima kuwe na maandalizi mazuri ya kuyaendea mafanikio  ya kupokea hatua mpya.
Kipindi cha wamama na majukumu ni kipindi ambachio hurushwa na n.y.u redio kila siku ya jumanne kuanzia saa kumi na moja za jioni hadi saa 12 na nusu za jioni ambapo wamama hupata fursa ya kujadili maswala mbalimbali yahusuyo familia.
Habari Na Ngurumo ya Upako.
 
Jumanne,July18,2017

MCHUNGAJI FURAHINI: KUWANA NA IMANI KUU NA KUMTEGEMEA MUNGU UNAINULIWA KATIKA MAISHA YAKO.

Watu wametakiwa kuwa na Imani kuu huku wakimtegemea Mungu ili waweze kufanikiwa katika maeneo mbalimbali Maishani.  
Hayo yamesemwa na Mchungaji Furahini John wakati akihubiri katika ibada ya chuo cha manabii iliyofanyika hii leo katika hema la kukutania kisongo Arusha ambapo amesema kuwa mtu akimtegemea Mungu katika maisha yake atapata thawabu kubwa sana maishani.





Aidha ameongeza kuwa watu wanakiwa kuzidi kuwa na Imani kwani kwa kufanya hivyo kupata majibu kwa wakati ni lazima.

kwa upande wake Mtume Eva Steven katika mahubiri yake amesema kuwa siku zote Mungu anajua ni wapi unaelekea kwani ndiye kiongizi.
Aidha huduma ya ngurumo ya upako ibada za katikati ya wiki ni Jumanne na Alhamisi ambapo watu kutoka maeneo mbalimbali huudhuria katika hema la kukutania kwa ajili ya kupokea uponyaji. 

Habari na Ngurumo ya Upako.



WATU MBALIMBALI WAMEALIKWA KUHUDHURIA IBAD YA CHUO CHA MANABII JUMANNE YA LEO 18/07/2017

kadinali wa Tatu WA huduma ya ngurumo ya upako mchungaji zimani gervas amewaalika watu kutoka sehemu mbalimbali kuhudhuria ibada ya katikati ya wiki inayofanyika hii leo  katika hema la kukutania kisongo arusha .
Akizungumza na redio n.y.u 99.3 fm ofisini kwake mapema leo asubuhi amesema kuwa katika ibada ya katikati watumishi wa mungu hupita katikati ya watu kwaajili ya kuwafungua watu kulingana ana mahitaji yao.
aidha amesema kuwa huduma ya ngurumo ya upako ipo kwaajili ya watu wote haichagui dini wala kabila kwani nguvu ya  mungu ipo kwaajili ya kuwahudumia watu wote.

Habari na Ngurumo ya Upako.





NABII MKUU MH DK GEODAVIE  AMEWATAKA WATU KUWA NA UWEZO MZURI WA AKILI ZA ROHONI NA AKILI ZA MWILINI.




Watu wametekiwa kuwa na akili za rohoni na mwilini ili waweze kufanikiwa
katika maeneo mbalimbali maishani.

Nabii mkuu Mh Dk GeoDavie  ameyasema hayo katika ibada ya jiji chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika hema la kukutania kisongo arusha ambapo amesema kila kitu kilichofanyika vizuri huwa kinakuwa na maandalizi mazuri.
Pia amesema kuwa katika maisha watu wanatakiwa waendeshe akili mbili za rohoni na akili za mwilini ili waweze kufanikiwa katika mambo mbalimbali maishani.
Katika ibada hiyo Nabii mkuu Mh Dk GeoDavie  ametangaza kuwepo hemani jumapili ijayo ambapo amesema itakuwa ni jumapili ya kusanyiko huku akiwagiza watu kuja na sadaka maalumu  kwa ajili ya kufanyika kichwa kwa akili za rohoni na akili za mwilini.
Nabii mkuu Mh Dk GeoDavie  ametoa wito kwa watu wote kuhudhuria ibada hiyo kwani itakuwa ni siku ya muhimu kwa kila Mtu

Kwa upande wa watu waliohudhuria ibada ya chuo kikuu cha manabii wamesema kuwa wamebarikiwa sana.

                                                                       Habari na Ngurumo ya Upako.




Wababa  wametakiwa kufika kwa wingi  siku ya jumapili katika ibada ya jiji itakayofanyika katika hema la kukutania kisongo Arusha  ambapo  ibada hiyo itaongozwa na Nabii Mkuu Mh Dk GeorDavie.

Hayo yamesemwa na wababa wa ngurumo ya upako wakati wakizungumza katika  kipindi cha wababa na majukumu kinachorushwa  na N.Y.U Redio kila siku ya ijumaa kwanzia saa 11 jioni.

Wababa hao akiwemo Jacob Mushi,Massawe pamoja  na Jonson Lazaro wamesema ujio wa nabii mkuu katikati yenu ni jambo la neema  na la Baraka sana kwa kila atakayefika kushiriki katika ibada hiyo.

Pia wamesema kutii maagizo kuna umuhimu mkubwa sana  na faida kwani wapo wengi sana waliofanikiwa kwa kuyatii maneno ya Nabii Mkuu Mh Dk Geor Davie.

Aidha ibada ya jiji itakayofanyika siku ya jumapili katika hema la kukutania kisongo Arusha itaongozwa na Nabii Mkuu Mh Dk GeorDavie  ambapo watu watakuja wakiwa  wamefunga pamoja na sadaka  ya unabii ya shilingi elfu 10.



Habari na Ngurumo ya Upako.


Watu wametakiwa kutoogopa kutokana na matatizo mbalimbali wanayokabiliana nayo maishani badala yake wamgeukie Mungu ambaye anamajibu ya kila mmoja.







Hayo yamesemwa na Mtumishi mwanafunzi Julieth Mwanyika wakati akihubiri katika ibada ya chuo cha manabii iliyofanyika katika hema la kukutania Ngurumo ya upako kisongo Ambapo alifundisha somo lisemalo”Geuka Maana Yesu ana Majibu yako”.

Akihubiri Mtumishi Julieth amesema kuwa inawezekana kuwa kuna watu wamepokea habari mbaya ikiwemo Magonjwa, Madeni, Umasikini, lakini pamoja na hayo hawatakiwi kuogopa kwa kuwa yupo Mungu anaweza kuwavusha katika mapito hayo.

Naye Mtume Eser Robert akihubiri ibadani hapo amesema kuwa ili mtu aweze kuzikabili Baraka zake maishani anahitaji nguvu, Imani, Fedha na Mikopo.

Kwa upande wake kadinali wa tatu wa huduma ya ngurumo ya upako Mchungaji Zimani Gervas aliwakumbusha watu kutoa sadaka maalum ya miezi miwili ya kupokea upako wa kukamilisha na kufanikisha malengo inayotolewa kila siku ya Alhamis kuanzia saa nne Usiku kwa muda wa mwezi wa sita na wa Saba.

Aidha Chuo cha Manabii ibada ya katikati ya wiki hufanyika siku za Jumanne na Alhamis ambapo watu kutoka sehemu mbalimbali huudhuria hemani kwa ajili ya kupokea uponyaji.

Habari na Ngurumo ya Upako.

KADINALI WA TATU WA HUDUMA YA NGURUMO YA UPAKO MCHUNGAJI ZIMANI GERVAS AWAKARIBISHA WATU KUHUDHURIA IBADA YA CHUO CHA MANABII HII LEO.
 

Akizungumza na N.Y.U Radio ofisini kwake Kadinali wa tatu wa huduma ya Ngurumo Ya Upako Mchungaji Zimani Gervas
amesema katika ibada za katikati ya wiki watu hufundishwa neno la mungu kwa kifupi na baada ya neno watumishi wa mungu waliochini ya Nabii mkuu Mh. Dk GeorDavie huanza kuwafungua watu kutoka vifungo vya mateso.

Ameongeza kuwa ibada ya leo itakuwa ni ya baraka, hivyo watu watapokea miujiza, maongezeko na hatua mpya katika kila eneo.

Aidha amesema kuwa huduma ya ngurumo ya upako ipo kwa ajili ya watu wote kwani haichagui dini, kabila hivyo nguvu ya mungu ipo kwa ajili ya kuwahudumia watu wote

Habari na Ngurumo ya Upako.

WATU WAENDELEA KUTHIBITISHA MANENO YA KINABII WANAYOTAMKIWA NA NABII MKUU MH. DK GEORDAVIE.

Watu mbalimbali wameendelea kuthibitisha maneno ya kinabii wanayotamkiwa Na Nabii Mkuu Mh. Dk GeorDavie kwani yameweza kuwatoa katika mateso mbalimbali yaliyokuwa yakiwasumbua kwa muda mrefu.
Hayo yamesemwa na Bi Happynnes Joseph mkazi wakati akizungumza na N.Y.U Radio ambapo amesema kuwa kwa kuamini nguvu ya mungu iliyopo katika madhabahu ya Ngurumo ya upako imeweza kumponya.  
Aidha Bi Happynnes amewataka watu wengine waendelee kuiamini nguvu iliyopo katika madhabahu ya Ngurumo ya upako kwani kupitia nguvu hiyo watu wengi wameponywa.

Habari na Ngurumo ya Upako.

 

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA KATIKA IBADA YA CHUO CHA MANABII HII LEO.

Watu wametakiwa kumtegemea mungu katika kila jambo kwani kwa kufanya hivyo kuna faida kubwa ya kuwawezesha kuvuka katika maeneo mbalimbali.

Hayo yamesemwa na mchungaji mwanafunzi wa vijana Suzan Nassary alipokuwa akihubiri kwenye ibada ya chuo cha manabii iliyofanyika katika hema la kukutania kisongo Arusha.
 
  Mchungaji mwanafunzi wa vijana Bi Suzan Nassary. 
 {Picha na Richard Shiyo}

Nae mchungaji Lidya peter amesema kuwa ni muhimu watu kuwa na mioyo ya shukrani pamoja na kutii ili waweze kufanikiwa katika maeneo mbalimbali.

https://www.facebook.com/lydia.peter.378
                                         Mchungaji Lidya Peter akihubiri leo hii. {Picha na Richard Shiyo}

Aidha watumishi wa mungu wanaotumika chini ya Nabii mkuu Mh Dk GeorDavie wamewafungua watu kutoka katika vifungo vya mateso.

                  Mwl. Mwanafunzi Annamesiah Masawe akihudumu leo hii.
                                             {picha na Richard Shiyo}

Ibada ya chuo cha manabii hufanyika kila siku za Jumanne na Alhamis ambapo watu kutoka sehemu mbalimbali ambapo watu uhudumiwa na watumishi wa mungu kwa ukaribu.

Habari na Ngurumo ya Upako.



WATU WAKARIBISHWA KUHUDHURIA IBADA YA KATIKATI YA WIKI YA CHUO KIKUU CHA MANABII.


Kadinali wa tatu wa huduma ya Ngurumo Ya Upako Mchungaji Zimani Gervas amewaalika watu kutoka sehemu mbalimbali kuhudhuria ibada ya katikati ya wiki inayofanyika hii leo katika hema la kukutania kisongo Arusha.

Akizungumza na N.Y.U Radio amesema kuwa katika ibada ya katikati ya wiki watumishi wa mungu hufundisha neno la mungu kwa kifupi na mara baada ya neno la mungu hupita katikati ya watu kwa ajili ya kuwafungua watu kulingana na mahitaji yao.

 



Ameongeza kuwa ibada ya leo itakuwa ni ya baraka, hivyo watu watapokea miujiza, maongezeko na hatua mpya katika kila eneo.

Aidha amesema kuwa huduma ya ngurumo ya upako ipo kwa ajili ya watu wote kwani haichagui dini, kabila hivyo nguvu ya mungu ipo kwa ajili ya kuwahudumia watu wote.

Habari na Ngurumo ya Upako.





...

No comments:

Post a Comment