Nashindwa hata niongelee vipi neno
tatizo.Sababu kila mmoja ana maana yake.Na matatizo yanatofautiana
kutoka kwa mtu hadi mtu.Familia hadi familia,ukoo hadi ukoo,jamii hadi
jamii.na taifa hadi taifa.Nchi za dunia ya tatu zikiwa na matatizo ya
maji safi na barabara nzuri.Mataifa ya dunia ya kwanza yanapitia makosa
kadhaa ili kutafta amani ya milele na upendo wa kweli.Jamii ya wafugaji
ikiwa na tatizo la ardhi kwa matumizi ya mifugo na wanyama.Jamii ya
wakulima inapitia makosa kadhaa ili kupata ardhi kwa matumizi ya mazao
na mashamba.Sote kwa nyakati mbalimbali tunakumbwa na shida
zisizoligana.Tunatenda makosa yasiofanana.Na muda mwingine tunakuwa hivi
kulingana na athari hasi ya mafunzo tuliyopata. Tulifundishwa
shule,mwenye akili ni yule asiyekuwa na matatizo ni yule asiyefanya
makosa.Mwenye vema nyingi za zoezi ni mshindi.Mwenye maksi kubwa za
mtihani ni wa kwanza.Mwenye makosa mengi ni mjinga ni wa mwisho hata
baada ya masahihisho picha hiyo haibadiliki kwa huyo mtu.Tuliaminishwa
hivyo tukasadiki hivyo.Kumbe hata kuamini hivyo kwa asilimia 100 ni
makosa bado.Kwa sababu mambo yanakawa kinyume tunapoingia mitaani.Huku
anayekosea sana na kujisahihisha ndiye mshindi, ndiye anayesogelea
mafanikio ndiye anayeitwa tajiri.Hakuna tajiri aliye na stori
ilinyooka.Kuna mahala alishindwa ,alikatishwa tamaa,aliogopa lakini
akapiga moyo konde na kuendelea. Umewahi kumsikia.Edson Thomas
aliyefanya majaribio ya taa 10,000 bila mafanikio.Taa ya 10,001 ndio
ikamletea heshima na utajiri.Au umewahi kusikia stori ya Abraham
Lincolin,Rais wa marekani aliyeshindwa biashara tatu wakati wa ujana,
akapigwa chini mara saba katika kampeni wakati wa kutafta nyasifa za
kisiasa?. Mpaka baadae ndipo anakuwa rais wa awamu ya 16 ya hilo taifa
lenye nguvu duniani.Hivyo hatuna haja ya kuogopa kukosea kwani haya
maisha yanaturejesha kwenye maana mpya kabisa ya neno tatizo au
matatizo. kosa au makosa.
1.''Kama hujawahi kukosea hujawahi kujaribu kitu kipya'' Albert Einstain
2.''Makosa ni kiashiria cha ukomo wa maarifa yako''Robert Kiyosaki
3.''Matatizo ni kipimo cha mtu na akili''Luther king jr
4.''Kila mbele ya tatizo kubwa pana fursa njema inakusubiri''
5.kukimbia tatizo hakulitatui bali kunaongeza umbali kati ya
tatizo na utatuzi
6.Mwanvuli haukati mvua ispokuwa unatupa ujasiri wa kusimama
katikati ya mvua,matatizo hayakwazi maisha isipokuwa yanatupa utashi wa kujikwamua.
7.Tatizo ni sawa na mashine ya nguo katika kazi na madadiliko,tegemea kufikichwa,kukunjwa,kusuguliwa mpaka uwapo
safi zaidi ya ulivyokuwa hapo mwanzo
8.Tatizo ni sawa na dirisha litakupa upeo wa mbali endapo
utalisogelea.
9.Matatizo ni kipimo unahitaji mafanikio kiasi
gani.Unavyoyatatua mengi, mafanikio yako yanaongezeka.
by rich voice
No comments:
Post a Comment