Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira imesema changamoto iliyopo
katika kupata taarifa sahihi za Wazanzibar wanaopata ajira katika
Taasisi za Muungano anuani ya makazi.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Kangi Lugola
amesema hayo bungebi jijini Dodoma leo Mei 30, alipokuwa akijibu swali
la Mbunge wa Welezo, Saada Mkuya (CCM).
Katika swali lake, Mkuya huyo alitaka kujua katika mambo yaliyokubalika katika mkakati wa kutatua changamoto za Muungano.
“Baadhi
ya changamoto hizo ni pamoja na kugawana ajira zilizopo katika Taasisi
za Muungano kwa asilimia 21 Zanzibar na 79 kwa Tanzania Bara, je ni kwa
kiasi gani mkakati huo umetekelezwa,” aliuliza Mkuya.
Akijibu
swali hilo Lugola amesema: “Changamoto iliyopo katika kupata taarifa
sahihi za Wazanzibar wanaopata ajira katika Taasisi za Muungano ni
kutoandika anuani zao za Zanzibar badala yake wanatumia anuani za mikoa
ya Tanzania Bara.”
by rich voice
No comments:
Post a Comment