Mamlaka
ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), juzi ilitangaza
kushuka kwa bei ya petroli na dizeli kwa asilimia 2.7 na asilimia 3.8;
na ongezeko la asilimia 0.09 kwa mafuta ya taa.
Taarifa
iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Nzingagwa Mchany ilisema
bei hizo mpya zitatumika Tanzania Bara kuanzia leo.
Hata
hivyo, kwa watumiaji wa mafuta yanayopitia katika Bandari ya Dar es
Salaam ni neema, lakini wa Bandari ya Tanga bei imeongezeka.
Mchany
alisema mabadiliko hayo ya yanatokana na kushuka kwa bei ya mafuta
katika soko la dunia na marekebisho ya bei yaliyofanywa na Ewura
kutokana na kubadilika kwa tozo za wakala na Serikali za mitaa katika
bidhaa hizo.
Ikilinganishwa
na tangazo la bei ya mafuta la Aprili 4 kwa mafuta yanayopitia katika
Bandari ya Dar es Salaam, bei ya petroli imepungua kwa Sh88 kwa lita
(asilimia 3.8) na dizeli Sh61 kwa lita (asilimia 2.75); huku bei ya
mafuta ya taa ikiongezeka kwa Sh2 kwa lita sawa na asilimia 0.09.
Tofauti
na wanunuzi wa rejareja, bei ya wale wa jumla upande wa petroli
imepungua kwa Sh100.91 kwa lita (asilimia 4.58), dizeli Sh73.71 kwa lita
(asilimia 3.52) na mafuta ya taa Sh10.49 kwa lita sawa na asilimia
0.51.
Mafuta
yanayopita Bandari ya Tanga bei kwa wanunuzi wa rejareja imeongezeka
kwa asilimia 0.14 kwa petroli na asilimia 0.71 kwa dizeli.
Lakini
wauzaji wa jumla bei imepungua kwa asilimia 0.46 (Sh9.8 kwa lita) kwa
petroli na asilimia 0.1 (Sh1.9 kwa lita) kwa dizeli.
“Hakuna
uingizaji mpya wa mafuta uliofanyika nchini kupitia Bandari ya Tanga,
lakini kutokana na mabadiliko ya bei ya Ewura kuna mabadiliko ya bidhaa
hizo tofauti na ilivyotangazwa Aprili 4,” alisema Mchany na kuongeza:
“Bei ya petroli itaongezeka kwa Sh3 kwa lita, huku dizeli ikiongezeka kwa Sh15 kwa lita.”
Kutokana
na kupungua kwa mafuta ya taa katika Bandari ya Tanga, Ewura
imewashauri watumiaji wa mikoa ya Nyanda za Juu kuchukua bidhaa hiyo
katika Bandari ya Dar es Salaam kwa bei elekezi.
Taarifa
ya Mchany inasisitiza kila kituo cha kuuzia mafuta kuchapisha bei
kwenye mabango yanayoonekana bayana na kituo kutoa risiti za
kielektroniki (EFD) kwa kila mauzo.
No comments:
Post a Comment