Mkuu
wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara amepewa onyo
kali na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kutoka na yeye kuingia uwanjani
kushangilia ushindi wa timu yake mara baada ya kumalizika kwa mchezo
kati ya Simba na Yanga uliochezwa Aprili 29, 2018.
Manara amepewa barua iliyomuonya kutokana na kukiuka sheria za michezo za ligi kuu mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
Mtendaji
Mkuu wa Bodi Ligi, Boniface Wambura ameeleza kuwa uamuzi huo umeafikiwa
katika kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kilichopitia
taarifa na matukio mbalimbali ya ligi msimu wa 2017/18 yanayoendelea
kulindima hivi sasa, ambapo kilibaini tukio la utovu wa kinidhamu kwa
afisa huyo.
“Katika
mechi namba 178 dhidi ya Yanga SC iliyochezwa Aprili 29, 2018 katika
uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, mara baada ya filimbi ya mwisho
kupulizwa aliingia uwanjani Haji Manara kushangilia ushindi wa timu
yake. Kitendo hicho ni cha ukiukwaji wa Kanuni ya 14(11) ya ligi kuu
kuhusu taratibu za mchezo, inayozuia wasiohusika kuingia uwanjani kabla,
baada na wakati mechi ikiendelea”, amesema Wambura.
Kwa
upande wake, Haji Manara ameonesha kulitambua kosa lake na kuiomba
radhi Bodi ya Ligi, Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), pamoja na
wadau wote wa soka, huku akieleza kuwa furaha ndiyo iliyompelekea yeye
kutenda kosa hilo.
“Muungwana
akivuliwa nguo huchutama..naomba radhi bodi ya ligi,TFF na wadau
wote..nilihemewa na furaha ndugu zangu..hakuna raha kwangu mm na kwa
mshabiki kama kumgalagaza mtani…it will never happen again..ila sijui
itakuwaje siku ya kukabidhiwa mwaliπππ @tanfootball #bodiyaligi ππ”
ameandika Haji Manara karika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.
Katika
Mechi hiyo ambayo ilihudhuriwa namashabiki wengi kutoka maeneo
mbalimbali nchini, Simba iliibuka kidedea baada ya kuichapa Yanga goli 1
ambalo lilifungwa dakika ya 37 na Erasto Nyoni.
No comments:
Post a Comment