Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga ameomba radhi kwa Rais Magufuli kwa niaba ya watu wa Iringa kwa kukosa kura 25 kipindi cha kampeni za uchaguzi mwaka 2015.
Balozi Maiga ameomba radhi hiyo leo kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa inafanyika katika uwanja wa Samora mkoani Iringa.
“Ilikuwa mwaka 2015 ulipokuja hapa katika kampeni yako yakuwa Rais wetu,Nakumbuka Mhe. Rais ulipata shida kidogo kupata wadhamini hapa Iringa Mjini ikabidi utoke nje ya mji ndiyo ukapata ila kura 25 tu kwa hapa mjini kura hazikupatikani tunakuomba radhi sana Mhe. Rais kwa kukosa busara hiyo. Lakini ulipokuwa hapa ulitoa ahadi kwa wana Iringa na umezitimiza ahadi ya kwanza ulisema Iringa itakuwa ni Makao Makuu ya Utalii ya mikoa ya Kusini hilo tumeshalifanya,” alisema Waziri Mahiga.
BY RICHARD SHIYO/RICH VOICE
No comments:
Post a Comment