Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amekataa
ombi la kuongeza mshahara kwa wafanyakazi iliyoombwa na TUCTA.
Akizungumza leo Mei 1 mkoa Iringa katika siku ya Wafanyakazi amesema
kuwa kwasasa fedha nyingi zinatumika kwenye miradi mikubwa ya maendeleo.
“Kwangu mimi ninafikiria hizi pesa tunazotoa kwa ajili ya elimu bure
ni nzuri kuliko fedha hizo kuzipeleka kuongezea mishahara, naona bora
kuwapa mikopo wanafunzi wa vyuo vikuu kuliko kuongezea wafanyakazi
mishahara,” amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa Mwaka huu wataendelea kutoa nyongeza
ya kawaida ya mishahara ya mwaka na wanataka wafanyakazi wote wapate
stahiki zao.
BY RICHARD SHIYO/RICH VOICE
No comments:
Post a Comment