Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,
ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM), amepewa tuzo
ya heshima na klabu ya soka ya Coastal Union ya jijini Tanga.
Coastal
Union wametoa tuzo hiyo kwa Ummy, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango
wake ambao ulifanikisha harakati zao za kurejea ligi kuu kuanzia msimu
ujao baada ya kufanikiwa kuwa miongoni mwa timu sita zilizopanda msimu
huu.
Tuzo
hizo ambazo zimetolewa na baraza la wazee wa timu hiyo chini ya
Mwenyekiti Salimu Bawaziri pia amekabidhiwa Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani pamoja
na wadau wengine.
Ummy
alijitolea kugharamia kambi za timu hiyo wakati wa michezo ya ligi
daraja la kwanza pamoja na kulipa mishahara na posho za viongozi na
wachezaji jambo ambalo liliongeza hamasa kwa wachezaji.
Coastal
Union ni miongoni mwa timu sita zilizopnda ligi kuu msimu ujao.
Nyingine ni Alliance Schools, Biashara Mara, KMC, African Lyon na JKT
Tanzania ambazo zitachukua nafasi za Ndanda FC na Majimaji FC huku
zingine zikiongeza idadi ya timu kutoka 16 hadi 20.
No comments:
Post a Comment