Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustine Mahiga
amesema Watanzania waishio nje ya nchi wanatuma zaidi ya Sh trilioni
moja nchini kwa mwaka.
Waziri
Mahiga ametoa taarifa hiyo bungeni jijini Dodoma leo Mei 23, wakati
akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/19.
“Watanzania
hao wamekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa taifa kwa kuwa baadhi
yao wamenunua nyumba zenye thamani ya Sh bilioni 29.7 kutoka Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC).
“Aidha,
katika sekta ya afya, timu ya madaktari wa Kitanzania waishio Marekani
kupitia taasisi ya afya, elimu na maendeleo ilitoa huduma ya afya bila
malipo na vifaa tiba,” amesema.
Pamoja
na mambo mengine, Waziri Mahiga amesema Tanzania kama nchi huru haiwezi
kuchaguliwa maadui na marafiki duniani na kwamba itaendelea
kushirikiana na mataifa mbalimbali duniani kulingana na jinsi
itakavyoona inafaa.
No comments:
Post a Comment