Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania(TFF) limewaondoa Waamuzi wawili kwenye orodha ya Waamuzi wa
Ligi ya Mabingwa wa Mikoa(RCL) inayoendelea kwenye vituo vinne vya
Geita,Singida,Rukwa na Kilimanjaro.
Waamuzi walioondolewa katika
orodha hiyo ni Seleman Nonga kutoka Arusha aliyekuwa katika kituo cha
Geita na Dadu Fadhil Msemo wa Kilimanjaro aliyekuwa kituo cha Singida.
Nonga ameondolewa baada ya
kuonyesha kiwango hafifu cha uchezeshaji ,kushindwa kumudu mchezo,kukosa
umakini,kutozingatia sheria ipasavyo kwa kipindi kikubwa cha mchezo na
kupata alama ndogo katika tathmini ya Wasimamizi kwenye mchezo namba A7
kati ya Kumuyange FC dhidi ya Ambassador.
Msemo ameondolewa baada ya
kuonyesha kiwango hafifu cha uchezeshaji ,kushindwa kumudu mchezo,kukosa
umakini,kutozingatia sheria ipasavyo kwa kipindi kikubwa cha mchezo na
kupata alama ndogo katika tathmini ya Wasimamizi kwenye mchezo namba C6
kati ya Temeke Squad dhidi ya Mtwivila City.
Waamuzi hao wawili wanatakiwa kuondoka kwenye vituo vya Geita na Singida leo Jumamosi Mei 12,2018.
TFF haitawavumilia waamuzi
watakaoendelea kuchezesha chini ya kiwango katika mashindano hayo ya RCL
pamoja na mashindano mengine yote kwakuwa TFF imejielekeza katika
uchezeshaji wa haki katika mashindano yake yote na TFF haitasita
kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayetaka kuharibu mashindano ya RCL.
No comments:
Post a Comment