NAIBU
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto dkt. Faustine
Ndugulile amethibitisha kuwa hakuna mtu aliyethibitika kuwa na ugonjwa
wa EBOLA hapa nchini wala hakuna ugonjwa huo hapa Tanzania.
Hayo
ameyasema leo jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari wakati
akitoa tamko kuhusu ugonjwa wa EBOLA kama ilivyodaiwa na baadhi ya
vyombo vya habari kuwepo kwa ugonjwa huo hapa nchini.
“Napenda
kuwatoa hofu watanzania kwamba hakuna ugonjwa wa EBOLA na wala hakuna
mtu aliyethibitika kuwa na ugonjwa huo, hivyo tuendelee na shughuli za
kujenga Taifa ila tunatakiwa tuchukue tahadhari za kujikinga juu ya
ugonjwa huu” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha,
Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa
EBOLA usiingie nchini Serikali imeweka vifaa vya kupima joto la mwili
(themo scaner) pia wapo wataalamu wa Afya ambao wanauliza hali ya
wageni wanaoingia katika mipaka yote inayoizunguka nchi yetu ili kuzuia
ugonjwa huo kuingia.
Dkt. Ndugulile amesisitiza kuwa, Serikali haijafunga mipaka ya nchi kwa sababu ya kujikinga na EBOLA.
“Tanzania
hatujafunga mipaka na hatuwezi kufunga biashara za mipakani ila
tumeimarisha ufuatiliaji wa watu wanaoingia nchini hususani maeneo ya
viwanja vya ndege na mipaka mingine yote.”
Mbali
na hayo Dkt. Ndugulile ameitaka mikoa yote iliyo mipakani kudhibiti
watu wote wanaoingia nchini kwa njia za panya ili kuepusha uingizaji wa
ugonjwa huo kwa wananchi huku akiwataka wafanyabiashara wa mipakani
kutoa ushirikiano ili kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani ambaye pia ni Afisa
wa kushughulikia magonjwa ya kuambukiza Dkt. Grace Saguti amesema kuwa
Wananchi wanatakiwa kupata elimu juu ya kujikinga na ugonjwa huo.
“Elimu
inahitajika ya kutosha kwa wananchi wote hasa katika kufichua wagonjwa
wa Ebola kama watagundulika hasa wanaotoka nje ya nchi ili kupata msaada
kutoka kwa watoa huduma za afya walio yao juu ya kujikinga na ugonjwa
huo.
No comments:
Post a Comment