Serikali imesema inapata tabu kukiri kuwa kuna hali ya njaa nchini kwa kuwa mvua zimenyesha za kutosha mwaka huu.
Kauli
hiyo imetolewa leo Mei 2, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji wakati akijibu swali la Mbunge wa
viti maalumu (CCM), Khadija Nasri Ally.
Mbunge huyo alitaka kujua kauli ya serikali kuhusu hali ya njaa na umaskini nchini.
Alisema
ripoti za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Taasisi ya utafiti
(REPOA), zimebainisha kuwa hali ya njaa na umaskini imeongezeka mwaka
huu ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Akijibu
swali hilo Dk. Kijaji amesema hali ya njaa nchini haipo kwani mvua za
kutosha zimenyesha na wananchi wana amani kwani hakuna uhaba wa chakula.
“Napata
tabu kusema kusema hali ya njaa imeongezeka ndani ya mwaka 2018 wakati
mfumuko wa bei za bidhaa zinazochangia upatikanaji wa chakula nchini kwa
mwezi Machi mwaka huu ulikuwa asilimia 3.9 pekee.
“Hii ni dalili kuwa hali ya njaa nchini haipo labda mbunge ametumia takwimu za miaka iliyopita mwaka 2016/17 ,” amesema.
by richard shiyo/rich voice
No comments:
Post a Comment