Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph
Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga
wakilakiwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mh. Freeman Mbowe mara baada ya
kuachiwa huru leo Alhamis Mei 10,2018 jijini Mbeya.
Awali Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe, mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda na viongozi
wengine wa chama hicho wamefika Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya
kuwapokea Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa
Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga.
Wawili hao wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao
Akihojiwa na kituo cha Redoa
cha Clouds Mwenyekiti wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe amesema wamepata
taarifa kutoka vyanzo vyao ambavyo hakuvitaja kwamba Mh. Joseph Mbilinyi
anaachiwa leo asubuhi kutoka Gereza la Ruanda ambako alikuwa akitumikia
kifungo cha Miezi mitano na mwenzake Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa,
Emmanuel Masonga
Sugu na Masonga walitiwa
hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26 katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais
John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka
jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
by richard shiyo/rich voice
No comments:
Post a Comment