Sunday, May 11, 2014

IBADA YA JUMAPILI TAREHE 11-05-2014

     Ilikuwa  Jumapili nyimgine ya baraka zaidi pale ambapo maelfu ya waumini wa Huduma ya Ngurumo ya Upako waliweza kufika na kupokea baraka za Mungu chini ya Hema la kukutania Kisongo Arusha ambapo,

Ibada hiyo iliyo ongozwa na Muasisi wa Manabii Tanzania Dr.GeorDavie ilikwenda mpaka majira ya saa mbili kasoro za usiku.

     Hata hivyo Nabii Mkuu wa Karne ya 21 na Muasisi wa Manabii Tanzania Dr.GeorDavie aliweza kuwatamkia Neno la Kinabii la wiki ambalo ni "WIKI YA KUTEMBEA KATIKA BARAKA TOFAUTI" ambapo pia Nabii Mkuu Mh.Dr.GeorDavie aliwataka WanaNgurumo wote waliofika katika hema la kukutania Ngurumo ya Upako yaani Chuo Kikuu cha Manabii Kujitamkia baraka kwa kille kila mmmoja alikuwa anataka iwebaraka kwake na Kuwaambia wakumbuke kuwa Neno la Nabii ni Sheria kwa kuamini neno alilolitamka Nabii Mkuu wa Karne ya 21 Nchini Tanzania Dr.GeorDavie na Ikawa hivyo.
Nabii Mkuu wa Karne ya 21 Mr.Dr.GeorDavie akiwatamkia maneno ya baraka Watoto waliohudhuria katika Ibada.
     Mara baada ya Mafundisho na kutoa maneno ya Kinabii Nabii Mkuu wa Karne ya 21 na Muasisi wa Manabii Tanzania Dr.GeorDavie aliweza kumkaribisha  Mtume Dr.Damas Mukasa ili aweze kutoa mafundisho kwa ufupi kwa waumini waliokuwa wamekusanyika katika Hema la kukutania Chuo Kikuu Cha Manabii Ngurumo ya Upako na Kwa hakika Mtume Dr.Damas Mukasa aliweza kufundisha barabara na watu walimuelewa na Kuzidi kujengwa kiimani zaidi.
Mtume Dr. Damas Mukasa.
Maelfu ya waumini wa Ngurumo ya Upako wakifuatilia Neno kwa Umankini.

    Sanjari na Maneno ya Kinabii yaliyotamkwa na Nabii Mkuu wa Karne ya 21 kutoka Tanzania Mh.Dr.GeorDavie pamoja na Mafundisho ya Mtume Dr.Damas Mukasa Ibada hii iliamabatana na Zoezi la kujenga msingi kwa mandalizi ya ununuzi wa Eneo kwa matumiz ya Huduma ambapo zoezi hilo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.


      Mara badaa ya hayo yote kufanyika ikaanza kazi ya kuwahudumia na kuwafungua watu wote waliokuwa wamekusanyika chini ya Hema la kukutania Kisongo Arusha kazi iliyofanya na Muasisi wa Manabii Tanzania Dr.GeorDavie kwa Maneno Machache Kazi kubwa na Nguvu ya Mungu iliyondani ya Nabii Mkuu Mh. Dr.GeorDavie ilimiminika na kuwaweka huru wote waliokuwa ndani ya vifungo vya movu shetani.


Maelfu ya waumini wa Ngurumo ya Upako wakiendelea Kupokea bila hata kujali ilivyokuwa usiku.
Kazi ya kufungua watu iliendelea hadi majira ya usiku.

Mara baada ya ushindi uliopatikana Muasisi wa Manabii Tanzania Mh.Dr. GeorDavie aliamua kucheza na kufarahipamoja na  waumini wa Ngurumo Ya Upako nakama inavyoonekana hapo chini...
Nabii Mkuu Mh.Dr.GeorDavie(Wapili mstari wa pili Katikati) akicheza pamoja na Waumini wa Ngurumo.
Maelfu ya waumini wa Ngurumo Ya Upako wakicheza na tumtukuza bwana pamoja na Nabii Mkuu Mh.Dr.GeorDavie.

Muigizaji Maarufu wa Filam Tanzania Pastor Emmanuel Miamba nae alikuwa miongoni mwa walioshiriki katika ibada hii na kupokea baraka za Mungu kutoka kwa Nabii Mkuu Mr.Dr.GeorDavie.
Muigizaji Maarufu wa Filam Tanzania Pastor Emmanuel Miamba akipanda Mbegu chini ya Miguu ya  Nabii Mkuu Mr.Dr.GeorDavie.Pia alitamkiwa kuzidi kuwa Star kimataifa zaidi.





TAZAMA JINSI MUASISI WA MANABII TANZANIA AKICHEZA NA WANANGURUMO KATIKA IBADA.

No comments:

Post a Comment