Thursday, June 5, 2014

CHATU AUWAWA KUTOKA KATIKA NYUMBA YA MTU JIJI ARUSHA

         
Ikiwa imepita takribani miezi miwili tangu Nabii Mkuu na Mwasisi wa Manabii Tanzania Mh.Dk.GeorDavie atangaze ushindi dhidi ya kazi na nguvu zote za wachawi na waganga wa kienyeji, mambo mbalimbali yameelendelea kutimia amabapo ni pamoja na hili la nyoka aina ya
chatu aliyesadikiwa kutumika katika imani za kishirikina kuuawa na wananchi katika eneo la Sakina jijini Arusha.
          Wakizungumza na N.Y.U blog kwa nyakati tofauti waliweza kuthibitisha na kuonyesha hasira kali kutokana na hali hiyo wakiwa katika eneo la tukio huku wakitumia mashoka na mapanga kumcharanga chatu huyo aliyekuwa amefungwa kitamba cheupe chenye maandishi mekundi
         Hatahivyo mmoja wa  mashuhuda alieleza kwamba mara baada ya kuonekana chatu huyo walimpigia simu mmiliki wa nyumba hiyo na alikuwa akisisitiza wasimuue chatu huyo kwani ni mtoto wake wa kwanza lakini hali hiyo ilizidi kuwagadhabisha mamia ya watu waliokuwa eneo hilo la tukikio na kuhitimisha kazi yao ya kumuangamiza nyoka huyo kama anavyoonekana katika picha.


No comments:

Post a Comment