Monday, June 9, 2014

UTHIBITIBISO WA MANENO KINABII ULIOTOLEWA NA MUASISI WA MANABII TANZANIA Mhe.Dr.GeorDavie JUU YA UPATIKANAJI WA MADINI KIRAHISI KWA WACHIIMBAJI(LOLIONDO)


Maelfu ya wakazi  Wilayani Loliondo na maeneo mbalimbali nchini wanaendelea kumiminika katika eneo kulikogundulika kuwa  na madini  aina ya dhahabu katika kijiji cha
mugongo kata Wilayani humo.

Wakizungumza  kwa nyakati tofauti na waandikshi wa habari baadhi ya wananchi wamesema kuwa tangu kugundulika kuwepo kwa madini katika kijiji cha mgongo idadi ya watu imekuwa ikieongezeka kijijini hapo kila kukicha.

Kwa  mujibu wa Diwani wa kata ya Samunge Jackson Sandea amesema kuwa hadi sasa kuna zaidi ya watu 8,000 na bado wanaongezeka na kubainisha kuwa idadi hiyo ya watu inaweza kuongezeka zaidi ya sasa.     

Hata hivyo Kugundulika kwa madini hayo ni Siku chache tu  baada ya Nabii Mkuu Dr.Geordavi kutoa unabii wa  siku 90  wa kufanikiwa kwa watu wanaochimba vito vya thamani.

Kwa upande wa mkuu wa Mkuu Wa Wilaya ya Loliondo Bwana Eliasi Wawalawi akizungumza na N.Y.U Radio mapema leo ameeleza kuwepo kwa madini hayo katika kijiji cha Mgongo Kata Ya Samunge Wilayani Loliondo.
Aidha tamko hilo la kinabii lililotolewa na nabii mkuu Dr.Geordavie limetia kablaya ya kumalizika siku tisini alizotoa hapo awali yakiambatana na kutimia kwa manaeno mbalimbali ya  kinabii aliyotoa ikiwemo unabii wa chombo kupoteza muelekeo ambapo hivi karibuni na kuwepo kwa mabadiliko ya hali ya Kigeographia .CLICK HAPA


No comments:

Post a Comment