HABARI ZA KITAIFA.

  Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Septemba 13

Ofisi ya Wakili wa Yusuf Manji, Hudson Ndusyepo Yavamiwa na watu wasiojulikana na Kutoweka na kabati la kutunzia nyaraka

Watu wanane wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wamevamia jengo la Prime House lililopo Mtaa wa Tambaza  na kufanya uharibifu wa mali za wapangaji.

Jengo la Prime House lina ghorofa tano lipo jirani na ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Ilala.

Mwandishi  ameshuhudia barabara ya kuingia eneo hilo ikifungwa kwa muda na polisi ambao walitumia magari yao kuziba njia na kuweka uzio wa  utepe wa rangi ya njano.

Jengo la Prime House lina ofisi za kampuni mbalimbali, zikiwemo za mawakili  wa Yusuf Manji ambazo zimevamiwa na wameondoka na nyaraka muhimu, duka la dawa na sehemu ya kufanya mazoezi gym.

Mmoja wa mawakili ambao wana ofisi katika jengo hilo, ambaye  hakutaka kutaja jina lake alisema  kwamba watu hao walipofika walimfunga mlinzi kwa kamba na kisha kuingia ndani kwa nguvu.

"Mlinzi ameniambia baada ya kuingia walipokuwa wakifanya upekuzi walikuwa wakisikika wakisema si huku tutazame ghorofa linalofuata si hili,” wakili huyo amemkariri mlinzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amethibitisha tukio hilo akisema limetokea kati ya saa nane na saa tisa usiku wa kuamkia leo.

Mwanafunzi Aliyenusurika Ajali Lucky Vicent Kutoa Ushahidi Mahakamani

Mwanafunzi   Wilson Tarimo, aliyenusurika katika ajali ya basi iliyoua wanafunzi 32 wa Shule ya Msingi Lucky Vincent ni miongoni mwa mashahidi 15 wa upande wa Jamhuri kwenye kesi inayomkabili mmiliki wa shule hiyo, Innocent Moshi.

Moshi anakabiliwa na tuhuma za makosa ya usalama barabarani ikiwamo kusafirisha wanafunzi bila kuwa na vibali muhimu.

Katika kesi hiyo namba 78 ya mwaka huu, Moshi pamoja na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Longino Nkana, jana walisomewa hoja za awali katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Desderi Kamugisha, Wakili wa Jamhuri, Khalili Nuda, alidai Jamhuri inatarajia kuwa na mashahidi 15 katika kesi hiyo, pamoja na vielelezo 12.

Mashahidi wengine ni Ofisa Kazi Mfawidhi wa Idara ya Kazi Mkoa wa Arusha, Wilfred Mdemi, Mohamed Matumula kutoka Kampuni ya Bima ya Zanzibar Insurance, Songoyi Jilala (askari wa usalama barabarani Arusha), Koplo Hamad (Karatu), Inspekta Shukrani (askari wa usalama barabarani Arusha), Koplo Saada (trafiki Arusha) na E.4312 PC Mugobe (trafiki Arusha).

Wengine ni Mkuu wa Polisi wa Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha (RTO), Nuru Suleiman, G 4130 PC Mwita (askari wa usalama barabarani Karatu), Ignatus Paul(Karatu), Leonidas Gerald (Morombo) na Hamis Omary mkazi wa Sombetini.

Wakili Nuda alitaja vielelezo hivyo kuwa ni kadi ya gari  namba  T 871 BYS, mkataba wa ununuzi wa gari, Barua ya RTO kwenda Sumatra ya Mei 8 mwaka huu, barua ya RTO kwenda Zanzibar Insurance ya Mei 8, mwaka huu na  taarifa ya Zanzibar Insurance ya Mei 9 mwaka huu.

Vingine ni taarifa ya Sumatra ya Mei 9 mwaka huu, taarifa ya idara ya kazi, taarifa ya ukaguzi wa gari, ramani ya eneo la tukio, maelezo ya mshitakiwa wa kwanza na maelezo ya mshitakiwa wa pili.

Wakili huyo aliiomba mahakama hiyo kutoa wito kwa mashahidi hao.

Akiwasomea hoja hizo za awali, Wakili Nuda alidai  katika shitaka la kwanza linalomkabili Moshi, ni kufanya biashara ya usafirishaji abiria bila kuwa na leseni ambapo kati ya Desemba 12 mwaka jana hadi Mei 6 mwaka huu, alitumia gari katika barabara ya umma  aina ya Mitsubishi Rossa T. 871 BYS, kubeba wanafunzi.

Alidai shitaka la pili ni kuruhusu gari hilo kutumika bila kuwa na bima kati ya Desemba 16 mwaka jana na Mei 6 mwaka huu.

Shitaka  la tatu ni kushindwa kuingia mkataba na mwajiriwa wake kati ya Juni Mosi mwaka jana hadi Mei 6, mwaka huu akiwa mmiliki  wa gari hilo alishindwa kuingia mkataba wa ajira kinyume na sheria za ajira na dereva wake, Dismas  Gasper ambaye kwa sasa ni marehemu.

Katika shitaka  la nne, Moshi anadaiwa kubeba na kuzidisha  abiria  13 ambako Mei 6, mwaka huu akiwa Mmiliki wa Kampuni ya Lucky Vincent, katika maeneo ya Kwa Morombo, aliruhusu gari hilo kubeba abiria 38 badala ya abiria 25.

Katika kesi hiyo, Nkama anakabiliwa na shitaka moja ambalo ni kuzidisha abiria katika chombo cha usafiri  ambako akiwa mwandaaji wa safari hiyo ya wanafunzi aliruhusu abiria zaidi ya 13 kupanda katika gari hilo ambalo lilipaswa kuwa na abiria 25.

Baada ya kusomewa maelezo hayo Moshi alikiri gari hilo kwenda Karatu likiwa halina bima huku Mwalimu Mkuu Msaidizi akikiri kuwa alizidisha abiria katika safari hiyo.
 
 

Tamko la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Baada ya Rais Magufuli Kugoma Kuwanyonga Wafungwa

 

 

Rais Amtembelea Meja Mstaafu Aliyepigwa Risasi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 12 Septemba, 2017 ametembelea hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo, Jijini Dar es Salaam na kumjulia hali Meja Jen. Mstaafu Vincent Mritaba aliyelazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wakati akiingia nyumbani kwake Ununio, Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Meja Jen. Mstaafu Mritaba alishambuliwa kwa risasi jana tarehe 11 Septemba, 2017 majira ya mchana na kisha kukimbizwa katika hospitali ya Jeshi Lugalo kwa matibabu.

Mkuu wa kituo cha tiba cha hospitali hiyo na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Brigedia Jenerali Paul Massawe amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa Meja Jen. Mstaafu Vincent Mritaba anaendelea vizuri baada ya madaktari kufanikiwa kutoa risasi alizopigwa mkononi, kiunoni na tumboni.

Meja Jen. Mstaafu Mritaba amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumjulia hali na kumuombea dua ili apone haraka.

Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jen. Venance Mabeyo pia ametembea wodi ya majeruhi na kuwajulia hali wagonjwa wanaotibiwa katika wodi hiyo na baadaye akawasalimu wananchi waliofika hospitali hapo kwa ajili ya kupata matibabu.

Mhe. Dkt. Magufuli amewapongeza Madaktari wa hospitali ya jeshi Lugalo kwa huduma za matibabu wanazotoa kwa askari na wananchi wengine na amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
12 Septemba, 2017
 
 
 

Spika aagiza Kubenea asakwe, Zitto afikishwe mbele ya kamati

Spika wa Bunge, Job Ndugai amemuagiza kutafutwa kwa namna yoyote Mbunge wa Ubungo(Chadema), Saed Kubenea apelekwe kesho kwenye Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ili ahojiwe kuhusu kauli aliyoitoa ya kumtuhumu Spika kuwa amedanganya idadi ya risasi alizopigwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),  Tundu Lissu.

Pia  Spika Ndugai ameagiza Kubenea na Mbunge wa Kigoma Mjini(ACT Wazalendo), Zitto Kabwe kupelekwa katika Kamati ya Bunge ya Maadili na Madaraka kwa tuhuma mbili tofauti                      

Zitto anatuhumiwa kutamka kuwa Bunge limewekwa mfukoni na muhimili fulani, wakati Kubenea ni kwa kumtuhumu Spika kusema uongo wa idadi ya risasi alizopigwa Lissu.

Spika Ndugai ametoa maagizo hayo bungeni mjini Dodoma leo Jumanne.
 
 
 

Katibu Mkuu CHADEMA Asimulia Jinsi Tundu Lissu Alivyo Vunjwavunjwa kwa Risasi

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema mwanasheria mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu ameumizwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake na kwamba alipigwa risasi nyingi tofauti na risasi tano zilizoelezwa.

Dk Mashinji amesema Lissu amevunjwa miguu yake, nyonga na mkono wa kushoto, jambo ambalo linawapa madaktari kazi kubwa na kuimarisha afya yake.

Kiongozi huyo amesema jana asubuhi Lissu alianza kusumbuliwa na kifua, jambo lililowalazimu madaktari kumwekea mashine za kumsaidia kupumua, hata hivyo anasema walizitoa baadaye na leo Jumanne ameamka salama.

"Bado najisikia uzito wa kuelezea jamii ya Watanzania hali ya kiongozi wetu Tundu Lissu, najua nina jukumu kubwa kama mtendaji wa chama kutaarifu umma juu ya hali ya Lissu inavyoendelea. Ni majonzi makubwa sana na kama kuna mtu katika taifa hili alifanya hicho kitendo anatakiwa ajitafakari sana. Mpaka jana asubuhi ameenza kupatwa na matatizo ya kifua kutokana na kulala kitandani muda mrefu, na kwa sababu mguu wake wa kulia umevunjwa vunjwa kwa risasi, nyonga yake pia mkono wake umevunjwa kwa risasi lakini 'inshallah' kama nilivyosema awali kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anayeamua kuchukua roho ya nani na aache ya nani", amesema Mashinji..

Amesema Lissu ameongezewa damu nyingi akiwa Dodoma na bado anaendelea kuongezewa huko Nairobi. Amesema madaktari wanajitahidi kuokoa maisha yake na kwamba ana imani kwamba watafanikiwa.

"Waswahili wanasema hujafa hujaumbika, kwa kweli wamemuumiza kwa hiyo ndugu zangu hiyo hali ya Lissu jana ilikuwa mbaya mpaka wakamuwekea mipira ya kupumulia lakini ilipofika wakati wa mchana hali yake ilikuwa inaendelea vizuri. Tunasafari ndefu ya kuhakikisha Lissu anapona, sasa hivi wamemtibu zile sehemu za ndani ambazo zingeweza kuhatarisha maisha yake kwa zile risasi zilizopita tumboni na sehemu nyingine", amesema Mashinji.
 
"Mhe. Lissu ni kweli tuliambiwa alipigwa risasi tano katika mwili wake lakini kulingana na hali ya mwili ulivyobomolewa yawezekana zilizidi. Leo ni siku ya tano akiwa anatibiwa hospitali na mpaka sasa hivi ameshafanyiwa oparesheni tatu nadhani itabidi kuzisitisha kidogo ili kumpa ahueni aweze kupumzika na yeye. Tulitegemea ingekuwa suala la kawaida tu yeye kwenda kutibiwa na kurudi lakini imekuwa tofauti. Msilie wala kusononeka kwa sababu Lissu bado yupo hai anaendelea kupigana na sisi, kuhakikisha kwamba anapona na kurudi kuendeleza ukombozi Watanzania ili kufikia uhuru wa kweli na mabadiliko ya kweli", amesisitiza Mashinji.

Kwa upande mwingine, Mashinji amesema wanajiandaa kisaikolojia kumpokea Lissu na hali ambayo atarudi nayo kwa kuwa hiyo ndiyo zawadi waliyopewa na Mwenyezi Mungu.
 
 

Mwanasheria Mkuu wa serikali amzungumzia Lissu

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju amefunguka kuhusu sakata la Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kupigwa risasi na watu wasiojulikana na kusema kuwa kwa sasa jambo hilo waachiwe polisi na vyombo vya usalama.

Akiongea leo bungeni George Masaju alianza kwanza kwa kutoa pole kwa Mbunge Tundu Lissu kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana na kusema serikali inalaani vikali kitendo hicho alichofanyiwa Tundu Lissu.

"Naomba kutoa pole kwa Tundu Lissu kwa majeraha aliyopata kutokana na kupigwa risasi na watu wasiojulikana sisi kama serikali tunalaani vikali jambo hili, kwa kuwa sasa jambo hili lipo kwa jeshi la polisi, tuviachie vyombo vya usalama naamini watafanya upelelezi kwa haraka" alisema George Masaju

Mbunge Tundu Lissu kwa sasa yupo nchini Kenya akipatiwa matibabu kufuatia kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 mjini Dodoma.

 

 

 

Breaking News: Jeshi la Polisi Lakanusha Kutuma Makachero Kumfuatilia Tundu Lissu Nchini Kenya

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika siku za karibuni kumejitokeza vitendo vya baadhi ya watu kutumia majina ama picha za watu na kuwahusisha na matukio ya kihalifu au matukio yanayohusiana na uhalifu kwa lengo la kujipatia umaarufu, kuwachafua watu hao au kuwakosanisha na jamii inayowazunguka.
Mnamo tarehe 11.09.2017 kupitia mitandao ya kijamii kulisambaa picha ya askari wa Jeshi la Polisi akihusishwa na muendelezo wa tukio la kujeruhiwa kwa risasi kwa Mhe. Tundu Lissu (MB) ambapo taarifa hiyo ilimtambulisha askari huyo kuwa ni kachero wa Kitengo cha Interpol na kwamba yupo jijini Nairobi nchini Kenya akifuatilia taarifa za Mhe. Lissu.
 
Jeshi la Polisi linapenda kukanusha taarifa hizo kuwa si za kweli na ni za uongo zenye lengo la kumchafua askari huyo na Jeshi la Polisi kwa ujumla. 

Askari huyo hayupo Nairobi kama ilivyoenezwa na picha iliyotumika ilipigwa hapa nchini tarehe 07.01.2017 kwenye sherehe ya mahafali ya mtoto wa kaka yake.
Kuhusiana na safari ya Nairobi, askari huyo alikuwa nchini Kenya kwa kozi ya kimafunzo kuanzia tarehe 04.09.2017 na kurejea tarehe 08.09.2017, huku Mhe. Lissu akipatwa na mkasa wa kujeruhiwa kwa risasi Tarehe 07.09.2017 na kusafirishwa kwenda Nairobi usiku wa kuamkia tarehe 08.09.2017.
Jeshi la Polisi linakemea vikali kitendo hiki chenye lengo la kumharibia maisha yake askari wetu, na linawataka wale wote waliohusika kusambaza au kutajwa katika taarifa hizo kuripoti kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kwa ajili ya mahojiano. 

Vilevile tunatoa onyo kwa wote wanaofikiri kuwa wanaweza kukaa na kupika habari ili waweze kuivuta jamii iwe upande wao na kuchafua upande wa serikali.
Suala hili la Mhe. Lissu lipo chini ya uchunguzi ili kuwabaini wote waliohusika na tukio hili na hatimaye kuwafikisha mahakamani. 

Ni vema wananchi na wanasiasa wakaliacha Jeshi la Polisi liweze kufanya kazi yake bila kuliingilia ili kuweza kupata ukweli wa jambo hili.
Jamii itambue kuwa Jeshi la Polisi linafanyakazi kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu za Nchi na kamwe halifanyi kazi kwa kuvizia. 

Endapo mtu yeyote anahitaji taarifa, tunayo mifumo yetu rasmi inayotuwezesha kupata taarifa tuzitakazo kupitia uhusiano tulionao ndani na nje ya nchi.
Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha upelelezi wa makosi ya mitandao (Cyber Crime Investigation Unit) linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wote waliohusika na kusambaa kwa taarifa hizi za uongo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya na badala yake mitandao hii itumike kwa ajili ya kuelimisha na kuihabarisha jamii juu ya masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Imetolewa na:
Barnabas David
Mwakalukwa – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi 
Makao Makuu ya Polisi.

 

 

 

Rais Magufuli Ahamisha Uwanja wa Michezo Dodoma

Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) Dodoma ilitenga Ekari 143 zilizopo Nara Barabara ya Singida nje kidogo ya mji wa Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa uwanja na kituo cha michezo kitakachojengwa kwa msaada wa serikali ya Morocco.

Waziri wa Habari, Mwakyembe amesema kuwa Rais Magufuli alitoa oda ya uwanja huo kuhamishwa na kupelekwa maeneo yaliyo karibu na mji wa Dodoma ili kutoka fursa kwa vijana na watoto kutumia uwanja huo pindi utakapokamilika kwani sehemu ambayo ilitengwa awali ni mbali sana kutoka mjini Dodoma.

"Tunamshukuru sana Rais wetu wa Tanzania Magufuli kwa kuikumbuka sekta ya michezo kwa kuomba Morrocco watujengee eneo changamani, walio wengi wanafikiri ni kiwanja cha mpira wa miguu lakini hapana hili ni eneo changamani litakuwa na michezo ya aina yote.
"Mwanzoni kama mnakumbuka tulipata eneo Nara eneo kubwa tu tuliomba ekari 150 tulipewa lakini Mhe. Rais Magufuli aliona kuna umbali kutoka Dodoma mjini mpaka Nara zaidi ya kilomita 70 akaona siyo rafiki, yeye angependa kuona vijana wake wa shule ya msingi na sekondari wakitoka shule wanakimbia uwanjani na umbali usiwe kikwazo" alisema Mwakyembe

Aidha Mwakyembe anadai kuwa Rais Magufuli aliagiza litafutwe eneo lingine

"Rais Magufuli aliagiza litafutwe eneo karibu na Dodoma mjini tujenge hiyo 'stadium' na kwa bahati nzuri sana agizo la Rais lilitekelezwa, tunamshukuru sana Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha tunapata eneo zuri kuelekea Dar es Salaam karibu na Nane Nane linaitwa Zuguni ambapo sasa tumepata ekari 300 na hizo zote tunazihitaji kwa sababu tunataka eneo hili changamani liwe la mfano katika ujenzi wa viwanja Tanzania kwa sababu tunataka baadaye kuwa na hoteli, kuwe na hosteli kwa vijana, tuwe na majumba makubwa ya michezo" alisisitiza Mwakyembe

Wahandisi, wabunifu na wataalam wa udongo kutoka nchini Morocco wameingia nchini Tanzania kufanya ziara na tathmini juu ya ujenzi wa eneo hilo changamani Dodoma

 

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO Jumanne,August 15,2017



 

  TUESDAY 15/08/2017

Makamba: Serikali haina nia ya kurudisha viroba

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesema Serikali haina nia ya kurudisha sokoni pombe zilizotengenezwa katika mifuko ya plastiki 'viroba' na kuwataka Watanzania kupuuza uzushi unaoenezwa kwamba pombe hizo zitarudi.



Makamba alitoa kauli hiyo jana, Jumatatu Agosti 14 alipotembelea eneo la Kimara Temboni lilipo ghala la kuhifadhi pombe mbalimbali ikiwamo viroba linalomilikiwa na Kampuni Thema.



Makamba alisisitiza kwamba Serikali uamuzi wake wa kuzuia pombe hizo upo palepale na haujabadilika hivyo watu waache kupotosha wenzao.



"Baada ya kupiga marufuku kuna kampuni zilikuja ofisini kuomba kuongezewa muda, lakini tuliwakatalia na kuwaambia waheshimu uamuzi uliotolewa sasa hizi tetesi ya kwamba vinarudi sokoni sijui zinatoka wapi," alisema Makamba.



Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli amesema  njia ya pekee kwa wafanyabiashara hao wa viroba wanaotakiwa kuifanya ili kupunguza hasara ni kubadilisha pombe hizo na kuziweka katika chupa zenye ujazo unaotakiwa.



Amesema kamwe Serikali haiwezi kurudi nyuma na kwamba mafanikio yameanza kuonekana kutokana na hatua hiyo.

 

 

TUESDAY 15/08/2017

Mambo 10 Ambayo Tanzania na Misri Zimekubaliana Kushirikiana baada Ya Rais Wao Kutua Nchini Jana





Tanzania  na Misri zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii katika maeneo makuu 10, ikiwemo kuimarisha uhusiano, ulinzi na kujenga kiwanda kikubwa cha nyama pamoja na kiwanda cha dawa nchini.

Pamoja na makubaliano hayo ya kiuchumi na kijamii, suala la matumizi ya maji ya Mto Nile halijapatiwa muafaka na mazungumzo yanaendelea kuwezesha kukamilisha matumizi yenye faida ya mto huo kwa nchi zote zinazohusika.

Aidha, Misri imempongeza Rais John Magufuli kwa utawala mzuri kwa namna anavyopambana na rushwa na ufisadi na kufafanua kuwa nchi hiyo (Misri) inaendelea kushirikiana na Tanzania katika mapambano hayo.

Makubaliano hayo takriban 10 yalielezwa jana Ikulu, Dar es Salaam na marais hao wawili wa Tanzania, Dk Magufuli na wa Misri, Abdel Fattah Al Sisi wakati wakizungumza na waandishi wa habari.

Rais Magufuli alisema wamekuwa na mazungumzo marefu mara baada ya Rais Al Sisi kuwasili jana mchana na ziara hiyo ikifanyiwa kazi kwa yale waliokubaliana, italeta manufaa makubwa kwa nchi hizo mbili.

“Tumezungumza mengi leo, nchi ya Misri ina historia kubwa katika dunia ya sasa, ustaarabu wa maisha ya binadamu ukiachia mbali binadamu wa kwanza inaelezwa aliishi Tanzania (Olduvai Gorge), wasanifu majengo wa kwanza waliishi Misri, ushahidi upo hata leo pyramids leo bado hakuna anayeweza kuzijenga.

“Vitabu vitakatifu vinaandika kuhusu Misri, Mtume Yesu alikimbilia Misri alipotaka kuuawa, ni eneo la kukimbilia wenye shida na sisi tutakimbiza shida zetu kwao ili atusaidie kuzitatua,”
alisema Dk Magufuli.

Alisema pamoja na kwamba hatujapakana kimipaka na Misri, lakini maji ya Mto Nile yameziunganisha nchi hizo mbili kwani chanzo cha maji kwenda Mto Nile ni pamoja na Mto Kagera na maji ya Ziwa Victoria ambalo asilimia 51 lipo Tanzania, 44 Uganda na tano Kenya.

Makubaliano 
Akielezea kuhusu maeneo ya makubaliano, Rais Magufuli alisema kwanza kutokana na historia ya mahusiano mema na ya muda mrefu baina ya Baba wa Taifa wa nchi hizo mbili; Mwalimu Julius Nyerere na Gamal Abdel Nasser, wamekubaliana kuimarisha mahusiano hayo kwa mustakabali wa nchi hizo mbili.

Dk Magufuli alisema wamekubaliana kuunda upya Kamisheni za Kudumu za Kiuchumi za Pamoja baina ya Tanzania na Misri ,ambazo ziliundwa awali na waasisi hao (Nyerere na Abdel Nasser) wa nchi hizo mbili. “Tumekubaliana hizi kamati (kamisheni) za kudumu ziundwe upya, wakutane mawaziri wan chi hizi mapema,” alisema Magufuli.

Eneo jingine ni kukuza biashara kati ya nchi hizo ambapo alisema kwa kuwa Misri inahitaji nyama na Tanzania ni nchi ya pili kwa mifugo mingi, nchi hiyo (Misri) itajenga kiwanda kikubwa cha nyama nchini ili wasafirishe nyama yenye viwango bora kwenda Misri.

Kiwanda hicho kikikujengwa, ajira kwa Watanzania zitapatikana, mapato na wafugaji watapata kipato zaidi kwa kuuza nyama moja kwa moja katika kiwanda hicho. Katika eneo la biashara, kwa sasa kiwango cha biashara baina ya Misri na Tanzania ni Dola za Marekani milioni 78.02.

Kiwango ambacho jana Rais Magufuli alisema ni kidogo na kinahitajika kuongezeka. Rais pia alieleza kuwa, Misri imekubali kuleta nchini teknolojia ya kilimo cha umwagiliaji nchini ili kukuza sekta ya kilimo.

Asilimia 95 ya nchi ya Misri ni jangwa na asilimia tano pekee huitumia kwa kilimo hasa cha umwagiliaji.

Alielezea eneo jingine kuwa ni sekta ya afya, ambapo amesema wamekubaliana na Rais Al Sisi kuendelea kuleta wataalamu na vifaa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali za Zanzibar na wamepanua wigo kwa kuongeza fedha kuwezesha operesheni za figo kufanyika kabla ya mwaka 2020.

Hata hivyo, hakueleza ni kiasi gani cha fedha walichoongeza. Katika sekta ya afya, pia wamekubali kujenga kiwanda cha kutengeneza dawa nchini hasa ikizingatiwa kuwa Misri ni moja kati ya nchi zenye viwango vikubwa vya ubora wa dawa duniani na hivyo ujenzi huo utaongeza ajira, afya, mapato na kukuza uchumi zaidi.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, uwekezaji wa kampuni za Misri nchini ni wa Dola za Marekani milioni 887.07 na umewezesha ajira nyingi.

Kuhusu utalii, Magufuli alisema wamekubaliana kuendesha sekta hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Misri na Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

Kwa sasa Misri inapokea zaidi ya watalii milioni 10 kwa mwaka na Tanzania ni wastani wa watalii milioni mbili kwa mwaka.

Ulinzi ni eneo jingine ambalo marais hao wawili wamekubaliana ili kuhakikisha amani kwa mataifa hayo inaimarika na Rais Al Sisi aliipongeza Tanzania inavyoshiriki kurejesha amani katika nchi za maziwa makuu na Rais Mtaafu Benjamini Mkapa kwa namna anavyosimamia amani Burundi.

Aidha, Tanzania pia itanufaika katika sekta ya elimu, ambapo marais hao wawili wamekubaliana kubadilishana walimu kwa lugha (Kiswahili, Kiarabu na dini) pamoja na IT.

Hata hivyo, pamoja na makubaliano hayo, Dk Magufuli alisema eneo la Mto Nile bado mazungumzo yanaendelea ili kuhakikisha kuwa maji ya Mto huo yanazinufaisha nchi zote zinazoguswa nao.

“Tunatambua maji ya Mto Nile ndio uhai wa Misri, tunatendelea katika mazungumzo ili mto huo umnufaishe kila nchi husika,” alisema Dk Magufuli.

Alieleza pia kuwa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein alipata nafasi ya kuongeza na Rais Al Sisi na kueleza changamoto kadhaa za Zanzibar na amekubali kuja tena nchini ili kufanya ziara Zanzibar ambako aliwahi kufika kibinafsi miaka 10 iliyopita.

Eneo jingine marais hao wamesaini makubaliano ya kupambana na rushwa na katika eneo hilo, Rais Magufuli alisema rushwa ni saratani inayohitaji nguvu ya pamoja kuimaliza huku Rais Al Sisi akiisifu Tanzania na Magufuli kwa namna wanavyopambana na rushwa na ufisadi na kueleza ataendeleza ushirikiano katika mapambano hayo.

Rais Al Sisi pia alieleza kuhusu makubaliano hayo na kusisitiza kuwa, Misri itaendelea kushirikiana na Tanzania katika miradi mikubwa ya maji kwa kujenga visima na kilimo cha umwagiliaji pamoja na maeneo ya afya.

“Namshukuru kaka yangu Rais Magufuli kwa makaribisho mazuri, ili ushirikiano uendelee namkaribisha Misri ili kuendelea kujadiliana namna ya kukuza maendeleo ya nchi zetu,” alisema Field Marshal Al Sisi.

Rais Magufuli alieleza kukubali kuitembelea Misri kwa wakati muafaka. 

.

 

 

TUESDAY 15/08/2017

Waziri Mkuu Awabana Maafisa Ushirika, Kilimo........Ataka wasimamie zao la tumbaku kwa umakini ili kumkoboa mkulima





WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka maafisa kilimo na maafisa ushirika wa mkoa wa Tabora wasimamie kwa umakini ukuzaji wa zao la tumbaku kuanzia msimu ujao.



“Mkakati wetu wa kuinua zao hili unaanza msimu ujao, ninaondoka Tabora lakini nataka kila mmoja wenu atumie nafasi yake kuelezea suala hili kwa kina kwa wakulima wa zao la tumbaku ili tubadilishe mfumo na tuweze kuwakomboa,” alisema.



Waziri Mkuu alitoa agizo hilo Jumapili, Agosti 13, 2017wakati akizungumza na watumishi wa idara za kilimo na ushirika na viongozi wa wilaya za mkoa huo kwenye kikao alichokiitisha ili awape maagizo maalum. Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia kilimo, Eng. Mathew Mtigumwe na baadhi ya watendaji kutoka wizara hiyo.



Aliwataka watendaji hao watumie vyombo vya habari vya ndani ya mkoa na vya kitaifa kuelezea mkakati mpya ambao serikali inao wa kuinua zao la tumbaku. “Tumieni vyombo vya habari kila mmoja apange ratiba kuelezea atafanya nini, toeni elimu kwa sababu vyombo hivi vinasikika hadi kwenye mikoa ya jirani,” alisisitiza.



“Afisa kilimo wa wilaya lazima ujue una wakulima wangapi, je wakulima wako kila mmoja analima ekari ngapi? Na katika ekari hizo, ana mahitaji ya pembejeo kiasi gani?” alisema.



“Afisa ushirika wa wilaya nawe hakikisha unasajili idadi ya vyama vya msingi (AMCOS) vilivyoko kwenye eneo lako, lazima ujue AMCOS ziko ngapi na zina wanachama wangapi. Afisa kilimo na afisa ushirika muanze kazi hiyo mara moja,” alisisitiza.



“Ulizeni mahitaji yao ni yapi, kwa kila mwanachama na kila AMCOS, kisha muziwasilishe kwa Mkuu wa Mkoa ili naye azifikishw kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo. Pale wizarani, tunataka Mkurugenzi wa Pembejeo ajue mahitaji ya kila mkoa ili pembejeo ziweze kuwasilishwa kwa wakulima miezi miwili kabla msimu wa kilimo haujaanza, kama ambavyo tumeagiza,” alisema.



Akifafanua kuhusu uagizaji wa mbolea, Waziri Mkuu alisema Serikali imeanzisha mfumo wa pamoja wa mbolea (bulk procurement) na akawataka wataalamu wa wizara ya kilimo wamalize mgogoro wa siku nyingi uliokuwepo baina yao na kiwanda cha mbolea cha Minjingu.



“Kumekuwa na maneno maneno kuhusu mbole ya NPK, lakini wakati sisi tunaidharau, wenzetu wa nchi jirani wanaongoza kwa kuagiza mbolea nyingi kutoka Minjingu. Acheni kuagiza mbolea hiyo kutoka nje ya nchi, tukachukue pale Minjingu,” alisisitiza.



Alisema mwenye kiwanda ameahidi kwamba akipewa oda ya mbolea, yeye atazisafirisha hadi kiwandani. “Hakuna haja ya kuwaumiza wakulima na mbolea za bei mbaya wakati tunayo hapa nyumbani na tena ya bei nafuu. Wenye makampuni ya kununua tumbaku wanauza mfuko mmoja kwa dola 70 sawa na sh.150,000 hii ya Minjingu yenye ubora uleule inauzwa sh. 60,000 kwa mfuko mmoja, tena zikiwa zimefikishwa wilayani.”



“Ninawasihi viongozi wa ushirika na wa wilaya tusaidiane kumuondoa mkulima kwenye utegemezi wa mikopo ya benki na badala yake tuwaelimishe wajiwekee akiba ya kumudu pembejeo za msimu unaofuata,” alisisitiza.



Alisema kama kutakuwa na ulazima wa kuingia kwenye mikopo, viongozi hao hawana budi kuhakikisha kuwa wanaisimamia kwa kikamilifu. “Kama mtaingia kwenye mikopo, lazima mjipange kuisimamia mikopo hiyo ili isije ikawarudisha nyuma wakulima wetu kwenye mfumo ambao ulikuwa unawaumiza,” aliongeza.



Akifafanua kuhusu ununuzi wa tumbaku, Waziri Mkuu alisema AMCOS ndizo zenye tumbaku na kwa maana hiyo ndiyo zitahusika na uuzaji. Katika kila wilaya, wekeni mfumo wa usimamizi kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama. Malori yakikamatwa na marobota yaliyouzwa nje ya mfumo, ni lazima hatua kali zichukuliwe,” alisisitiza.



“Ninasema hakuna mazungumzo tena nje ya AMCOS, ni kwa kampuni ya ununuzi au kwa mtu binafsi. Na kuanzia sasa, Associations za tumbaku zimefutwa. Mkuu wa Mkoa na wakuu wa wilaya hakikisheni hakuna associations kwenye zao la tumbaku, tunataka kila mmoja akanunue kwenye AMCOS na kila mkulima asajiliwe kwenye AMCOS,” alisisitiza.



Alisema Serikali ilivunja Chama Kikuu cha Ushirika Kanda ya Magharibi (WETCU) kutokana na ubadhirifu uliokuwa ukifanywa na viongozi wa chama hicho na kwamba hivi sasa kutakuwa na WETCU mbili ambapo ya kwanza (WETCU I) itahusika na wilaya za Kaliua na Urambo na ile ya pili (WETCU II) itahudumia wilaya za Sikonge, Uyui, Nzega na sehemu ndogo ya Tabora Manispaa.



Alisema hatua hiyo imechukuliwa ili kuwe na vyama vikuu viwili vyenye AMCOS chache lakini zenye uwezo wa kuwafikia wakulima, kusikiliza mahitaji yao na kutatua matatizo yao. WETCU ya zamani ilikuwa na AMCOS 214 na haikuweza kuwafikia wakulima wote.



IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMATATU, AGOSTI 14, 2017.

 

 

 

HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI YA APRIL 22 .


 

 

 JUMAMOSI YA APRIL 22

RAIS MAGUFULI: WATANZANIA WAMETESEKA VYA KUTOSHA......FANYENI KAZI USIKU NA MCHANA KUKAMILISHA HII BARABARA .

Rais Magufuli ameitaka kampuni ya Nyanza inayoshughulikia ujenzi wa barabara ya mkoani Kigoma kuanza kufanya kazi usiku na mchana kwa kuwa wapo baadhi ya wananchi hawajahi kuona lami maisha yao yote mpaka wanakufa.



Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo wakati akihutubia wakazi wa Kakonko mkoani Kigoma katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kibondo mpaka Nyakanazi yenye urefu wa kilomita 50 kwa kiwango cha lami.



"Wananchi hawa wanahitaji barabara ya lami wameteseka tangu dunia iumbwe, wako watu hawajui rangi ya lami, wapo watu hapa wamezaliwa, wamezeeka hawajui rangi ya lami ikoje. Kwa sababu hawajawahi kuona barabara ya lami katika maisha yao, kwa hiyo nataka hii lami ianze na mjipange kweli mfanye kazi usiku na mchana", amesema Rais Magufuli.



Pamoja na hayo Rais Magufuli amewaagiza makandarasi kufanya kazi ipasavyo na wasipofanya hivyo watachukuliwa adhabu kali zidi yao.



"Kwa bahati nzuri mimi kufukuza makandarasi ni kama kunywa chai, sasa asije akanirudisha kule nilipokuwa kwa sababu sasa ni Baba wa wote lakini nilipokuwa Waziri nilikuwa nafukuza tu, kwa kupitia bodi ya makandarasi nilikuwa nafuta wakandarasi na mimi nikuombe Prof. Mbalawa usiwe mpole. Makandarasi watakao kuwa wanafanya kazi hovyo hovyo, pole pole chukua 'action' ili kusudi kama kashindwa kufanya kazi ya ukandarasi akafanye nyingine hata ya kuvua samaki", amesisitiza Rais Magufuli.



Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amewataka wananchi kibondo na kasuru wa mkoa wa Kigoma na watanzania wote kwa ujumla kudumisha ulinzi na usalama katika maeneo yao wanayoishi ili kupunguza au kumaliza kabisa matatizo ya kihalifu yanayotokea.

 

 

 Thursday, July 20, 2017


TUNDU LISSU JANA ALITOA KALI........NI BAADA YA KUGOMA KUTOKA MAHAKAMANI AKIHOFIA KUKAMATWA NA POLISI


Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu  jana  aligoma kutoka katika chumba cha mahakama kufuatia kuwepo kwa tetesi kuwa kuna baadhi ya polisi wametumwa kumkamata kiongozi huyo. .



Lissu alifika mahakamani hapo jana asubuhi kwa ajili kusimamia kesi ya migogoro ya ndani ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) iliyokuwa ikisikilizwa na Hakimu Proches Mushi.



Katika kesi hiyo, Kamati ya Utendaji ya CWT wilaya imefungua kesi dhidi ya Katibu Mkuu wa CWT, Yahaya Msulwa wakimtuhumu kwa matumizi mabaya madaraka.



Hata hivyo wakijadili muda wa kurudi tena kwa kesi hiyo, Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, (TLS) alisema kuna polisi waliovalia kiraia waliokuwa wakimngojea nje ili wamkamate na kumsafirisha kwenda Dar es Salaam.



Habari za kutaka kukamatwa kwa Lissu zilisikika  asubuhi katika mitandao ya kijamii baada ya kutumiwa ujumbe kuwa kuna maaskari waliovalia kiraia wanataka kumkamata.



“Mheshimiwa naomba kesi hii isisomwe tarehe 23 kwa sababu sitakuwepo nchini, natarajia kwenda Uganda kwenye kikao cha vyama vya Afrika Mashariki vya mawakili,”alisema na kuongeza:



“Lakini pia nimepewa taarifa kuwa hapo nje kuna polisi wananisubiri nikitoka wanikamate na kunisafirisha kwenda Dar es Salaam hivyo huenda tarehe hiyo (Julai 23) nisiwe huru kuhudhuria kesi.”



Akijibu maombi hayo Mushi alisogeza kesi hiyo hadi Septemba 27-29 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.



Mara baada ya kesi kuahirishwa, Lissu akafanya mkutano na waandishi wa habari ndani ya ukumbi wa mahakama hiyo na kudai hatatoka mahakamani hapo ili aone kama polisi wana uwezo wa kuingia na kumkamata.



“Leo asubuhi nimepata taarifa kutoka Dar es Salaam kwa mama watoto wangu kwamba polisi walikuja nyumbani kwangu kunitafuta na wakaelezwa kwamba yuko Dodoma kwa muda wa siku tatu,” alisema.



“Baada ya hapo wasamaria wema walinitaarifu kuwa Jeshi la Polisi Dar es Salaam limewaomba wenzao wa Dodoma wanikamate pindi tu nitakapotoka hapa na kunirejesha Dar es Salaam.”



Alipoulizwa sababu inayofanya polisi watake kumkamata, Lissu amesema ni kutokana na maoni yake aliyoongea juzi ya kuukosoa uongozi wa Rais Magufuli.



“Rais Magufuli na chama chake wameshindwa siasa na wanachofanya sasa ni kutumia mabavu lakini wao kama Chadema kamwe hawataogopa wala kukaa kimya kwani kazi yao si kumsifia Rais bali ni kumkosoa anapofanya vibaya,”amesema.



Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki alisema hakuna sheria yoyote inayowaruhusu polisi kumkamata wakili akiwa katika shughuli zake mahakamani.



“Nakaa nione kama watavunja sheria ya kuja kunikamatia hapa hapa mahakamani. Nimeshazoea kukamatwa tangu mwaka huu uanze nimekamatwa mara nne,”alisema.



Baada ya kukaa mahakamani kwa saa nne, alifika Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa na kumweleza Lissu kwamba Jeshi la Polisi Dodoma halina taarifa yoyote wala mpango wowote wa kumkamata.



“Hatujapokea taarifa yoyote wala maelekezo yoyote ya kukukamata kutoka makao makuu. Hata ingekuwa hivyo tungeshakukamata kwa sababu muda wa mahakama umekwisha. Kwa sasa hivi yamebakia majengo tu kwa hiyo uwe huru uendelee na shughuli zako,” Mambosasa alimwambia mbunge huyo.



Baada ya Mambosasa kuondoka katika mahakama hiyo, Lissu naye aliondoka katika eneo hilo.

 

Thursday, July 20, 2017


SERIKALI KUWASHUGHULIKIA WANAOTOA MATAMSHI YA KICHOCHEZI


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itawashughulikia watu wote wanaotoa matamshi ya kichochezi nchini bila ya kujali nyadhifa zao.

Amesema ni vema watu wakawa makini na kijiepusha kutoa matamshi ambayo yataathiri mfumo wa maisha kwa wananchi wengine.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumatano, Julai 19, 2017) wakati wa ibada ya mazishi ya mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe Bibi Linnah Mwakyembe iliyofanyika wilayani Kyela.

Alisema Serikali haitavumilia kuona baadhi ya watu wakitoa matamshi ambayo hayana tija kwa jamii na badala yake yanalenga kuwavuruga wananchi na kuchochea migogoro.

”Tutashughulika na watu wote wanaotoa matamshi ya kichochezi, popote walipo bila ya kujali uwezo wao, vyeo vyao na mamlaka walizonazo.”

Pia aliwaomba viongozi wa dini waendelee kuliombea Taifa na viongozi wake na kwamba Serikali inawategemea na iko pamoja nao. 




Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo baada ya Askofu wa Kanisa la Evarinjerical Brother Hood, Rabison Mwakanani kuonya vitendo vya baadhi ya watu kumtukana Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli.

Alisema ni vema watu hao wakajifunza namna ya kuwasilisha hoja zao bila ya kutumia lugha za matusi.
“Rais Dkt. Magufuli amefanya mambo mengi makubwa kwa ajili ya maendeleo. Wanaofanya hivyo wasidhani kama wanamtukana Rais tu bali wanawatukana Watanzania wote waliomchagua wakiwemo viongozi wa dini.”

Pia aliwaomba wananchi kufanya maandalizi mapema kwa sababu wote ni wapitaji, hivyo waandae roho zao kwa kuacha kufanya dhambi na maovu yote ili wawe na mwisho mwema. 

Vile Vile Waziri Mkuu aliwaomba wananchi wote washirikiane kwa pamoja kumuombea Dkt. Mwakyembe na familia yake ili Mwenyezi Mungu aweze kuwafariji katika kipindi hiki kigumu.

“Wajibu wetu sote ni kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema. Tunajua kwa sasa Dkt. Mwakyembe yuko katika wakati mgumu, namuhakikishia kwamba hayuko peke yake kwani Serikali iko pamoja naye katika kipindi hiki kigumu.”

Naye, Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai alimpa pole Dkt. Mwakyembe huku akiitaka familia kuendelea kuwa na upendo kama ule uliokuwepo wakati wa uhai wa marehemu Bibi Linnah.

Kwa upande wake, Mtoto mkubwa wa marehemu, George Mwakyembe alisema anaamini mama yao, alijiandaa na kifo hicho kwa kuwa alikuwa mchamungu. 

“Mama alikuwa na ratiba kila siku ifikapo saa nne usiku lazima afanye ibada, Hivyo nina matumaini makubwa kupitia Uchamungu wake, Mwenyezi Mungu atamuweka mahala pema.”



ADC NAO WAMPINGA TUNDU LISSU




Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC) wameitaka Chadema itoe msimamo wake kuhusu kauli ya mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu kutaka jumuiya za kimataifa zisitishe misaada kwa Tanzania.

Katibu Mkuu wa ADC, Doyo Hassan amesema kama huo hautakuwa msimamo wa Chadema ,Lissu anapaswa kuomba radhi.

Amesema kauli ya kutaka misaada isitishwe hailengi kuwatakia mema Watanzania.

"Tunadhani matatizo yetu ya ndani ni vema tukapambana nayo kuliko kutangazia ugomvi wako kwa mtu asiyekuhusu.’’

"Kwa kauli hii hizi za Chadema ni wazi wameshindwa mapambano ya ndani na sasa wanafikiria njia nyingine ambazo ni hatari zaidi katika nchi yetu,"amesema Hassan.

Amesema kama Chadema imeshindwa kupambana na CCM na Serikali yake ni wazi wawaeleze wafuasi wao kuliko kutoa matamshi ambayo yanahatarisha ustawi wa taifa letu.




HABARI ZILIZOPO KATIKA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI YA JULY 20







Jumatano,July19,2017

RAIS MAGUFULI ATOA SIKU 14 KWA WAMILIKI WA VITUO VYOTE VYA MAFUTA NCHINI.

Rais John Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vyote vya mafuta nchini, kuhakikisha wanaweka na kutumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD) na atakayekiuka agizo hilo atafutiwa leseni ya biashara yake.
 













Rais Magufuli ametoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Kigoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa KM 154 huku akiwataka mawaziri wenye dhamana kuhakikisha wanafuatilia maagizo hayo kuanzia sasa.

 "Wanaolalamika kukosa mafuta waendelee kufanya hivyo, ni mara mia tukose mafuta kuliko kuwa na wafanyabiashara wanaokwepa kodi", amesema Rais Magufuli.
Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amepiga marufuku wananchi kutozwa kodi kwa mzigo wenye uzito wa tani moja anapousafirisha kutoka wilaya moja kwenda nyingine.

Habari: Kitaifa 

RAIS MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA KAGOMA-BIHARAMULO-LUSAHUNGA YENYE UREFU WA KILOMETA 154.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Barabara ya Kagoma-Biharamulo-Lusahunga imegharimu Sh 190 bilioni.
Waziri Mbarawa ametoa tamko hilo leo wakati wa uzinduzi wa barabara hiyo mbele ya umati mkubwa wa watu ambao wamehudhuria uzinduzi wa barabara hiyo ya  kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 154.
 

Akizindua ujenzi wa barabara hiyo leo Rais John Magufuli amesema kwamba Biharamulo imeshika nafasi ya pili kwa umasikini na wananchi wanafanya ulinganisho na hali ilivyo tofauti katika wilaya jirani ya Chato.
 
Kwa upande wake Mbunge wa Biharamulo, Oscar Mukasa amesema wanaunga mkono msimamo wa Rais kupiga marufuku wanafunzi wanaobeba mimba kuendelea na masomo na wameanzisha shule ya wasichana ya bweni kuunga mkono kauli yake.
Habari: Kitaifa

TRA YAMKANA NGELEJA SAKATA LA FEDHA ZA ESCROW, YADAI JUKUMU LAKE NI KUPOKEA KODI NA SIO FEDHA ZA KASHFA 

Februari 2014, Ngeleja ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Sengerema (CCM) aligaiwa Sh. milioni 40.4 na mfanyabiashara maarufu James Rugemalira ambaye mwanzoni mwa mwezi alifikishwa mahakamani akikabiliwa na
mashtaka 12, yakiwamo ya kughushi na utakatishaji fedha.


Waziri wa Nishati na Madini wa zamani Ngeleja ni mmoja kati ya watu waliopokea mgawo wa fedha zinazodaiwa kuwa zao la kashfa ya Tegeta Escrow, lakini akatangaza kuzirejesha kwa TRA Jumatatu iliyopita.
Hata hivyo, wakati Ngeleja akithibitisha kwa risiti mbele ya waandishi wa habari kuziingiza fedha hizo katika akaunti ya TRA, mamlaka hiyo imesema haizitambui. TRA imesema haina mpango wowote wa kufuatilia fedha hizo kwa sababu shughuli yake ni kukusanya kodi. 
Akizungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa TRA, Richard Kayombo alisema mamlaka hiyo inahusika na kuhakikisha serikali inakusanya kodi stahiki na siyo urejeshaji wa fedha za kashfa kama Escrow.
Kayombo alitoa ufafanuzi huo wakati alipoulizwa na Nipashe juu ya utaratibu rasmi uliopo wa urejeshaji wa fedha hizo endapo wanufaika zaidi wa mgawo wa Rugemalira watataka kufuata nyayo za Ngeleja.
Akifafanua zaidi juu ya suala hilo, Kayombo alisema TRA haihusiki na fedha zilizochotwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow kwa kuwa hazikuwa mali yake.
Aidha, Kayombo alisema TRA haiwezi kuzizungumzia fedha hizo kwa kuwa hazijawahi kuwa mali yake na kuelekeza watafutwe wenye fedha hizo kwa ufafanuzi zaidi. 
“Fedha za Escrow zinaihusu vipi TRA? Tunawezaje kukaa na kuzungumzia fedha ambazo si zetu?” Alisema Kayombo. “Mimi nashauri watafutwe wenyewe wazungumze kama wanataka kurejesha… siyo sisi.” 
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu aliiambia Nipashe wiki iliyopita kuwa uamuzi wa Ngeleja kupeleka fedha za hizo TRA unazua maswali zaidi kwa kuwa alipewa na Rugemarila, na viongozi wa awamu ya nne ya serikali walisema siyo za umma bali mtu binafsi. 
Lakini akizungumza jijini Jumatatu iliyopita Ngeleja alisema amerejesha mgawo huo kwa TRA kwa kuwa pamoja na sababu nyingine, ili kujiweka kando na kashfa.
Alisema aliyetoa mgawo huo ameshakamatwa na Takukuru na ana kesi inayoendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Huku akionyesha stakabadhi ya malipo ya Benki ya CRDB tawi la Tower, Ngeleja alisema pia “nimeamua kurejesha fedha hizi hata kama aliyenipa msaada bado ni mtuhumiwa, kwa vile hajathibitika kupatikana na hatia, kwa sababu sitaki kuwa sehemu ya kashfa au tuhuma hizo.” 
“Nimesononeshwa na kufadhaika sana kuona kuwa msaada niliopewa sasa unahusishwa na tuhuma.” 
 Alisema alipokea mgawo huo Februari 12, 2014 na Januari 15, 2015 alilipa kodi kwa TRA kiasi cha Sh. 13,138,125 ikiwa ni sawa na asilimia 30 ya msaada huo aliopewa. 
Hakusema ni kwa nini ulipita muda mrefu kati ya kupokea na malipo ya kodi.
Baada ya Ngeleja kurejesha fedha hizo palikuwa na wito kutoka kwa wanasiasa na wanaharakati waliotaka wote waliopata mgawo huo kurejesha fedha hizo kwa TRA kama alivyofanya waziri huyo wa zamani.
 

MASHTAKA 12
Rugemalira na mwenzake, mmiliki wa Kampuni ya Pan African Power (PAP), Harbinder Singh Sethi walisomewa mashtaka 12 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Julai 3.
Mashtaka hayo ni pamoja na ya kugushi, utakatishaji fedha na kusababisha hasara ya dola zaMarekani milioni 22.1 na Sh. bilioni 309.4 kwa serikali.
Novemba 26, 2014, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliwasilisha mjini Dodoma ripoti ya uchunguzi wa kashfa Tegeta Escrow ambapo ilisema Sh. bilioni 306 zilichotwa kutoka Benki Kuu kinyume cha sheria.
Mwenyekiti wa kamati hiyo wakati huo, Zitto Kabwe alisoma ripoti na kulithibitishia Bunge kwamba viongozi na wafanyakazi wa Serikali, wafanyabiashara, viongozi na taasisi za dini, mabenki na watu binafsi walihusika katika ufisadi.
Ripoti ya PAC ilianika orodha ya waliopata mgawo huo kuwa mbali na Ngeleja ni aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa zamani, Andrew Chenge ambao kila mmoja alipata Sh. bilioni 1.6.
Wengine ni ofisa katika Ofisi ya Rais wakati huo, Shabani Ngurumo aliyepewa Sh. milioni 80, Jaji wa Mahakama Kuu, Eudes Ruhangisa alipata Sh. milioni 404.25 na aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco), Dk. Enos Bukuku, aliyepewa Sh. milioni 161.7.
Katika ripoti hiyo Waziri wa Nishati na Madini wa serikali ya awamu ya tatu, Daniel Yona, Mbunge wa zamani wa Sumbawanga Mjini, Paul Kimiti, aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Emmanuel Ole Naiko na Jaji wa zamani wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Aloisius Mujulizi walitajwa kupatiwa Sh. milioni 40.4 kila mmoja.
Wengine ni ofisa wa TRA, Lucy Apollo Sh. milioni 80.8, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Rita), Philip Saliboko Sh. milioni 40.2, maaskofu Methodius Kilaini Sh. milioni 80.9 na Eusebius Nzingirwa Sh. milioni 40.4, Padri Alphonce Twimannye Sh. milioni 40.4, maofisa wa Rita Placidus Luoga Sh. milioni 121.2 na Theophil Rugozobwa Sh. milioni 323.4.

BAJETI WIZARA
Mgawo waliopata wabunge, maofisa wa serikali na viongozi wa dini kutoka kwa Rugemalira unatosha bajeti ya mwaka mzima ya miradi ya maendeleo ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Nipashe imegundua.
Katika miaka mitatu iliyopita ya bajeti (2014/15, 2015/16 na 2016/17), wizara hiyo ambayo kwa sasa iko chini ya Waziri Dk. Harrison Mwakyembe, ilitengewa bajeti ya Sh. bilioni tatu kila mwaka, ikiongoza wizara zote 18 kwa kuwa na bajeti ndogo zaidi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Wakati wizara hiyo ikiambulia Sh. bilioni moja (theluthi ya bajeti yake ya maendeleo) hadi inapofika robo tatu ya mwaka wa bajeti katika miaka hiyo mitatu, imebainika Sh. bilioni 4.77 zinazodaiwa zao la kashfa ya uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow walizopatiwa waheshimiwa hao zingetosha kugharamia kikamilifu miradi ya maendeleo ya wizara hiyo kwa mwaka mzima na ‘chenji’
ya Sh. bilioni 1.7 ikabaki.
Katika mwaka uliopita wa fedha, kwa mfano, kati ya Sh. bilioni tatu zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wizara hiyo, ni Sh. bilioni 1.19 tu (asilimia 40) ndizo zilizokuwa zimetolewa hadi Aprili 30, mwaka huu kwa mujibu wa Dk. Mwakyembe.
 Chanzo: NIPASHE

 

JUMANNE 18/07/2017

 NEMC YAANZA KUFUMULIWA HUKU VIONGOZI WAKE WAKITUMBULIWA .

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Januari Makamba amefanya mabadiliko makubwa kwenye Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC).



Akizungumza jana Jumatatu, Julai 17, Makamba alisema amebaini mazingira ya rushwa katika kutengeneza vyeti ambavyo havijafuata mchakato stahiki na urasimu.
Mengine ni kutokuwa na lugha nzuri kwa wateja na kuwatisha ili watoe chochote na kuzitumia kampuni binafsi za watumishi wa NEMC kufanya kazi za ukaguzi/uhakiki wa ndani ya NEMC kwa kisingizio cha kutokuwa na watumishi wa kutosha.
Pia amewasimamisha kazi  Manchare Heche, Deus Katwale, Andrew Kalua na  Benjamin Dotto  huku wengine wakiendelea kuchunguzwa wakati wizara ikiendelea kupokea taarifa za ziada.
Pia Waziri amefanya mabadiliko ya wakuu wa kanda;
Jafari Chimgege, aliyekuwa Kanda ya Mashariki, sasa atakuwa Mkuu wa Kanda ya Dodoma.
Goodlove Mwamsojo, aliyekuwa Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu-Mbeya, sasa atakuwa Mkuu wa Kanda ya Mashariki-Dar es Salaam.
Dk Ruth Rugwisha, aliyekuwa Mkuu wa Kurugenzi ya Sheria, sasa atakuwa Mkuu wa Kanda ya Ziwa Mwanza;
Dk Vedastus Makota, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano, sasa atakuwa Mkuu wa Kanda ya Kusini - Mtwara;
Joseph Kombe, aliyekuwa Mkuu wa Kurugenzi ya Utafiti na Mipango anakwenda kuwa Mkuu wa Kanda ya Kaskazini-Arusha.
Dk Menard Jangu aliyekuwa Kanda ya Arusha anarudishwa Makao Makuu ya NEMC kuwa Kaimu Mkuu wa Kurugenzi ya Utafiti na Mipango.
Jamal Baruti, aliyekuwa Mkuu wa Kanda ya Ziwa, anarudi Makao Makuu NEMC.
Lewis Nzari aliyekuwa Mkuu wa Kanda ya Kusini –Mtwara, sasa anakuwa Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

MAGAZETI YA JUMANNE LEO JULAI 18,2017





 

 BREAKING NEWSSSSSSSSS.

TFF Yamwachia Huru Mkuu wa Kitengo cha Habari wa klabu ya Simba Haji Manara







Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemuachia huru Mkuu wa Kitengo cha Habari wa klabu ya Simba Haji Manara kuendelea na majukumu yake kama kawaida.



Hayo yameweka wazi na Mwenyekiti wa Kamati ya nidhamu Abasi Tarimba katika mkutano wake na waandishi wa habari mchana wa leo.



Manara alifungiwa na Shirikisho hilo baada ya kubainika utovu wa nidhamu wa kutoa matamshi yasiyo na  staha kwa viongozi wa TFF pamoja na vyombo vya uongozi wa mchezo huo ambapo alihukumiwa muda wa miezi 12 na kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni tisa adhabu iliyotolewa na Makamu  Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya TFF Wakili msomi Jerome.

 

 

 

Kampeni‘MagufuliBaki’yaanzishwa........Mikutano kufanyika nchi nzima



 Rais John Pombe Magufuli ameendelea kupongezwa na wananchi pamoja na Taasisi za kiraia mbalimbali kutokana na misimamo yake na kazi kubwa anayoifanya ya kupigania rasilimali za nchi, kwa masilahi ya wanyonge na masikini.



Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti leo, Julai 17, 2017 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Masjid Ridhwaa, Alhaj Suleiman Seif Nassor na aliyekuwa mgombea wa CCM wa Ubunge Jimbo la Sengerema kupitia kura ya maoni, Laurence Mabawa.



Wakati akizungumza na wanahabari, Alhaj Nassor amesema bodi hiyo imemamua kumpongea Dkt. Magufuli kutokana na kazi nzuri anayofanya tangu alipoingia madarakani.



Kwa upande wake Mabawa, amesema licha ya kumpongeza Rais Magufuli, ameandaa kampeni kabambe inayojulikana kama ‘Magufuli Baki’ inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni kwenye mikoa yote nchini, ambapo kupitia mikutano wananchi wenye nia njema watamuomba rais abaki katika msimamo wake wa kuwatetea wanyonge na masikini.



“Kampeni ya Magufuli Baki itahusisha mikoa yote ya Tanzania kwa kuwafikia wananchi wakiwemo wanafunzi wa sekondari kwa kufanya mikutano yenye nia njema ya kumwomba Rais abaki kwenye msimamo wake, kampeni hii itawapa fursa wananchi kutoa maoni yao kuhusu utendaji kazi wake iwe kwa kupongeza au kukosoa,” amesema.



Katika hatua nyingine, Mabawa amelaani baadhi ya wanasiasa na wananchi wanaotoa lugha za maudhi na kejeli kwa watu wanaojitokeza hadharani kumpongeza Rais Magufuli na serikali yake.



“Niombe TCRA kuwachukulia hatua kali wote wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuwatolea maneno ya kejeli na kuudhi watu wanaojitokeza kumpongeza Rais,” amesema.



 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema safari ya Watanzania kuachana na nguo za mitumba imewadia kutokana na uwepo wa viwanda vya kutengeneza nguo nchini.

Pia amesema uwepo wa viwanda hivyo utasaidia wakulima wa pamba kupata soko la uhakika hivyo amewataka walime pamba ya kutosha ili viwanda vipate malighafi.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo   Jumamosi, Julai 15, 2017 wakati alipotembelea kiwanda cha nyuzi cha Namera kilichoko Gongo la Mboto na kiwanda cha nguo cha Nida kilichopo Ubungo Dar Es Salaam.

Alisema viwanda vya kutengeneza nguo nchini ni ushahidi tosha kwamba nchi iko njiani kuondokana na matumizi ya nguo za mitumba kwa kuwa nguo nyingi zitakuwa zinatengenezwa nchini, hivyo kupatikana kwa bei nafuu.

Alisema kwa sasa wanunuzi wa pamba hawana sababu ya kwenda kuuza nje ya nchi na badala yake wauze katika viwanda vya ndani ili vizalishe nguo za kutosha zitakazouzwa nchini kwa gharama nafuu.

“Pamba yote inaweza kuchakatwa nchini, hivyo hakuna haja ya kuiuza nje ya nchi. Natoa wito kwa wakulima wetu wa pamba walime mazao ya kutosha kwa sababu soko la uhakika ipo na hii ndio safari ya mwisho ya mitumba.”

Awali Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha saruji cha Lake kinachozalisha saruji ya nyati ambapo aliwapongeza wawekezaji wote nchini kwa kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa ya uchumi wa viwanda.

Katika kiwanda hicho ambacho kinazalisha tani 700,000 kwa mwaka kimeajiri watu 2000 na kinalipa kodi ya  sh. bilioni 81.312 kwa mwaka, Waziri Mkuu aliwataka watumishi wake wawe waaminifu, wafanye kazi kwa weledi na wawe waadilifu.

Pia Waziti Mkuu alitoa wito kwa wamiliki wa viwanda vyote nchini kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi waishio katika maeneo ya karibu na viwanda sambamba na kulipa kodi kwa wakati na kwa viwango sahihi.





 

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi   amelazimika kukesha ofisini kwake akiwahudumia wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani waliowasilisha matatizo mbalimbali kuhusiana na ardhi.



Waziri Lukuvi aliingia ofisini majira ya saa mbili asubuhi siku ya Ijumaa lakini akajikuta akilazimika kufanya kazi hadi saa tisa usiku wa kuamkia  jana Jumamosi.



Wananchi 189 wenye matatizo na kero za ardhi aliitikia wito alioutoa waziri Lukuvi mwezi Juni, akiwataka watu wote katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani, wenye matatizo ya ardhi, kujiorodhesha ofisini kwake pamoja na anwani zao na angepanga siku ya kushughulikia matatizo hayo yeye mwenyewe binafsi.



Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara, sehemu kubwa ya wakazi hao walilala nje ya ofisi za wizara hiyo jijini Dar es Salaam wakisubiri kuonana na waziri Lukuvi.



Wananachi wengi wenye matatizo na kero za ardhi waliokesha na Lukuvi walitokea Bagamoyo, Kibaha, Mkuranga, Kibiti na Dar es salaam.



Wananchi hao wamesifu hatua hiyo ya Waziri Lukuvi kukutana nao ana kwa ana na kuzitatua kero zao za ardhi kwa kuwa haijawahi kutokea.



Francis Kamara, mkazi wa Ilala jijini Dar es salaam, amemuomba Waziri Lukuvi awawajibishe watumishi ambao wanakwamisha jitihada zake hadi kusababisha yeye kukutana na wananchi moja kwa moja.

 

 Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 16



BREAKING NEWS: MATOKEA KIDATO CHA 6 MWAKA 2017 YAMETOKA.....BOFYA HAPA KUYATAZAMA
 Baraza la Mitihani la taifa (Necta) leo limatangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha sita.
==>>Bofya hapo chini Kuyatazama au cliki hii picha kutazama


 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya July 15