Monday, May 5, 2014

IBADA YA JUMAPILI TARE 04-O5-2014

  


Maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha na maeneo mbalimbali walikusanyika katika Hema la kukutania Chuo Cha Manabii Kisongo Arusha, ambapo waliweza kupokea na kufunguliwa kutoka katika vifungo mbalimbali vya muovu shetani.

     Hata hivyo Nabii Mkuu wa Karne ya 21 na Muasisi wa Manabii Tanzania Mh. Dr.GeorDavie aliweza kuwatamkia Neno la Kinabii la wiki ambalo ni "WIKI YA KUSAFISHWA JINA LAKO"Kutoka kwa wote walio kusema vibaya kwani wao hawakujui zaidi ya Mungu na hivyo basi wataanza kukupenda wenyewe.
     Sanjari na hilo pia Muasisi wa Manabii Tanzania Mh. Dr.GeorDavie alweza kuendelea na somo la "KEEPING UP WITH GOD KINGDOM STANDARDS " yaani KWENDA NA VIWANGO VYA SERIKALI YA UFALME WA MUNGU ambapo waumini wa Huduma ya Ngurumo ya Upako walizidi kujengwa katika Kweli ya Neno la Mungu na Kuzidi kutambua nini maana ya Mamlaka ya Serikali Tukufu ya Ufalme wa Mungu.

Muasisi Mkuu wa Manabii Tanzania Mh.Dr.GeorDavie akifundisha somo la KEEPING UP WITH GOD KINGDOM STANDARDS.
       Hata hivyo katiaka kuendelea kuthibitisha Mamlaka aliyonayo Muasisi wa Manabii Tanzania Mh.Dr.GeorDavie kutoka kwa Mungu ya kuwafungua watu na Kuwaponya kutoka katika Vifungo na Mateso ya Muovu shetani aliweza kuruhusu watu kutoa shuhuda apambo aliweza kusimama Mama mmoja aliyekuwa anaumwa kansa na kwa neno moja tu la Kinabii aliwza kupona na hata sasa ni mzima kabisa kama anavyo onekana katiaka picha chini.
Mama aliyeponywa kansa kwa neno moja tu alilotamkiwa na Muasisi wa Manabii Tanzania Mh. Dr.GeorDavie akionyesha makovu baada ya kupona kabisa.
Mama aliyeponywa Kansa akipanda mbegu miguuni mwa Mwasisi wa Manabii Tanzania Mh.Dr.GeorDavie.
                 

No comments:

Post a Comment