Tuesday, April 29, 2014

Urusi yawekewa vikwazo vingine na nchi za magharibi

Marekani na Umoja wa Ulaya zimewawekea vikwazo maafisa kadhaa   na makampuni ya Urusi ili kuiadhibu nchi hiyo kwa sababu ya kuhusika  na matukio ya nchini Ukraine.
   Hata hivyo vikwazo hivyo havitaulenga uchumi wa Urusi kwa jumla na pia hakuna uhakika iwapo vitaiathiri nchi hiyo.
Nchini Urusi kwenyewe imetanda  faraja kwamba hatua hizo hazikufika  mbali kama ilivyohofiwa.
   Hatua hizo ni pamoja na kuwapiga marufuku watu kadhaa kuingia katika nchi za magharibi na kuzizuia mali zao.Watakaoathirika ni wale waliopo  karibu na serikali ya Urusi.
   Viongozi wa nchi za magharibi wanatumai kwamba watakaobanwa na vikwazo hivyo hatimaye watamshinikiza Rais Wladimir Putin arudi nyuma katika hatua anazozichukua juu ya Ukraine ili kuundoa mvutano.
Rais Putin  amevipuuza vikwazo hivyo vipya,hata hivyo inakumbuka kwamba awali Marekani na Washirika wake waliweza tutangaza kuiondoa Urusi katika mataifa yenye utajiri mkubwa zaidi duniani kiviwanda yaani G8.
   

No comments:

Post a Comment