Friday, May 18, 2018

Korea Kaskazini na Marekani: Kwa nini Kim Jong-un anamuogopa Donald Trump

Kim Jong-un (L) talking with South Korea's President Moon Jae-in (R) before the inter-Korean summit at the Peace House building on the southern side of the truce village of Panmunjom on 27 April (picture released by North Korean state media)\
Rais wa Marekani Donald Trump ametoa matamshi yanayokinzana na ya mshauri wake wa masuala ya usalama wa taifa, akisema mfumo wa Libya wa kumaliza zana za nyuklia hauwezi kutumiwa nchini Korea Kaskazini.

Pendekezo la John Bolton liliighadhabisha na kuitia wasiwasi Korea Kaskazini ambayo ilitisha kujitoa kwa mkutano na Trump wa mwezi ujao.

Bw Trump amesema anaamini mkutano huo utafanyika.
Mwaka 2003 kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi alikubali kuachana na mpango wake wa silaha za nyuklia ili apate kuondolewa vikwazo na mataifa ya Magharibi.


Hata hivyo aliuawa na waasi walioungwa mkono na nchi za Magharibi miaka kadhaa baadaye, mfano ambao ulionekana kumtia wasi wasi kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Pyongyang ilionya Jumatano kuwa huenda isihudhurie mazungumzo hayo ambayo yanapangwa kufanyika nchini Singapore tarehe 12 mwezi Juni.

Rais Trump alisema nini?

Huku Bolton akitazama, Rais Trump alisema: "Mfumo wa Libya si mfumo tuko nao kabisa wakati tunafikiri kuhusu Korea Kaskazini."
Makubaliano ambayo Bw Trump alikuwa akizungumzia na Kim Jong-un ni kitu ambacho Kim atakuwepo, atakuwa nchini mwake, ataiongoza nchi yake na nchi yake itakuwa tajiri sana.

"Ukiangalia Korea Kusini, huu utakuwa mfumo sawa na wa Korea Kusini kimaendeleo... ni watu wanaojitahidi sana."
Kuhusu mkutano uliopangwa, Trump alisema: "Hakuna kilichobadilika na Korea Kaskazini tunachokifahamau, hatujaambiwa chochote."

Korea Kaskazini inaonaje suala hili?
Pia Alhamisi, Korea Kaskazini ilisema haitarejea kwenye mazungumzo na Korea Kusini hadi pale masuala tata kati yao yatasuluhushwa.
Pyongyang imeghadhabishwa na kuendelea kwa mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini ambayo inayaona kama matayarisho ya uvamizi.
Ilifuta mazungumzo ya ngazi ya juu na Korea Kusini mapema wiki hii.
Kwenye taarifa mpatanishi mkuu Ri Son-gwon alikosoa mamlaka za Korea Kusini kwa kukosa ustaarabu kufuatia hatua ya kumruhusu raia wa Korea Kaskazini aliyekimbilia Korea Kusini kuzungumza kwenye bunge mjini Seol.

Korea Kaskazini inaonekana kuweka shinikizo kwa Marekani na Korea Kusini na kukataa mazungumzo hadi matakwa fulani yatimizwe.

Ni kwa nini mfumo wa Libya unazungumziwa?

Tangazo la Korea Kaskazini kuwa huenda ikajitoa kwa mkutano na Marekani lilinyooshea kidole mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani John Bolton.
"Hatufichi hisia zetu dhidi yake," ilisema tarifa ya Jumatano, ambayo iliandikwa na naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Korea Kaskazini Kim Kye-gwan.
Korea Kaskazini ilikuwa ikimaanisha mahojiano ya Bolton aliyoyafanya akiufananisha na hali iliyotokea Libya katika kumaliza zana za nyuklia
Mwaka 2003 Kanali Muammar Gaddafi alikubali kuachana na mpango wake wa kustawisjha silaha za maangamizi makubwa kwenye tangazo lililoishangaza dunia.
Vikwazo vingi vya Marekani dhidi ya Libya viliondolewa ndani ya miezi michache na uhusiano wa kidiplomasia ukarejeshwa.
Lakini mwaka 2011 Gaddhafi alipinduliwa na waasi wakiungwa mkono na majeshi ya mataifa ya shirika la kujihami la nchi za Magharibi Nato.
Baadaye alikamatwa na kuuawa na vikosi vya waasi.

No comments:

Post a Comment