Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako,
amewajia juu baadhi ya watumishi wa serikali ambao wanatabia ya
kuwafukuza kazi walimu wakuu wa shule ambao hutoa matokeo mabaya katika
mitihani ya Taifa.
Ndalichako
alisema hayo wakati akijibu hoja za wabunge kuhusu bajeti ya wizara
yake na kuongeza watumishi hao hasa maofisa elimu, wanajukumu la
kusimamia elimu katika eneo husika na sio kuwatupia lawama walimu pindi
matokeo yanapokua mabaya.
“Hiyo
sio sawa ni uonevu kwa wakuu wa shule kwa sababu na wenyewe wana
viongozi juu yao, kwa nini wao ambao wanatakiwa kuwasimamia
wasiwajibishwe, ninaagiza maofisa elimu wafanye kazi yao vizuri, utakuta
mtu ana shule tano unashindwaje kuzisimamia, kwa hiyo katika hili
serikali itahakiksha tunaimarisha usimamizi ikiwa ni pamoja na kuondoa
viongozi ambao ni mizigo” alisema Ndalichako
Ndalichako
aliongeza kwamba kama serikali inachukua hatua kubwa ili kuimarisha
ubora wa elimu lakini baadhi ya watendaji hao wamekua wakirudisha nyuma
jitihada hizo na serikali haitasita kuchukua hatua kwa watendaji hao.
by richard shiyo/rich voice
No comments:
Post a Comment