Naibu
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ametoa wito
kwa wabunge kutojihusisha na vitendo vya kingono na wafunzi wa vyuo
vikuu na wawaache wasome.
Pia
ametoa rai kwa wanafunzi na wananchi kwa ujumla kutoa taarifa kwa
mamlaka husika pindi wanapopata taarifa za walimu na wahadhiri wa vyuo
vikuu kuwafelisha wanafunzi kwa kutaka rushwa ya ngono.
Kauli
hiyo ya OleNasha imekuja baada ya Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga
(CCM) kusema kuwa baadhi ya wahadhiri wanajifanya ni vidume vya mbegu
katika kuwafelisha wanafunzi hao.
Aidha, Naibu Waziri huyo amesema serikali imelipokea suala hilo na haina uvumilivu kwa vitendo hivyo.
“Pia
mwanafunzi hadi ahesabike kuwa amefeli haitokani na mtazamo wa mwalimu
mmoja tu, kuna taratibu zimeweka kupitia ‘marks’ (alama) ambazo amepata
kutokana na kazi zake ili kuamua amefaulu au amefeli. Hata kama ilitokea
mwalimu mmoja amefanya vitendo hivi, hii haiwezi ikaathiri ufaulu kwa
vitendo hivi.
“Vyuo
vikuu ikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), vina taratibu
maalumu ya kushughulikia masuala haya ya unyanyasaji wa kijinsia lakini
wanafunzi wengi hawatumii msaada huu. Tunawasihi kama watapata matatizo
kama haya waende kwa mshauri wa wanafunzi (dean of student),” amesema.
No comments:
Post a Comment