Wednesday, April 2, 2014

UTHIBITIBISO WA MANENO KINABII ULIOTOLEWA NA MUASISI WA MANABII TANZANIA Mh.Dr.GeorDavie JUU YA JIJI LA ARUSHA.

 
 Ilikuwa mwishoni mwa mwaka 2013 ambapo MUASISI WA MANABII TANZANIA Mh.Dr.GeorDavie aliweza kufanya Ziara katika eneo la maduka la SHOP RITE jiji Arusha na kutoa Unabii kwa maendeleo ya jiji la Arusha na kuwatamkia maelf ya watu waliokuwa wamefika katika eneo hilo kuwa na afya njema.

     Miongoni mwa maneno aliyoyatamka katika ziara hiyo SHOP RITE ni pamoja na kutanuka kwa Jiji la Arusha nakuwa na maeneo makubwa ya kibiashara pia alitamka mafanikio ya kutosha kwa kila mfanyabiasha wa jiji la Arusha na kurahisisha mzunguko wa fedha na aliweza kutoa baraka za kupata uponyaji wa afya njema kwa kila mmoja aliwezakufika.
    Hata hivyo MUASISI WA MANABII TANZANIA Mh.Dr.GeorDavie aliweza kuwatamkia baraka viongozi wote wa Serikali na viongozi wote wa Dini kwa ujumla ndani ya Arusha.
TAZAMA SEHEMU YA VIDEO YA ZIARA HIYO ALIYOIFANYA MUASISI WA MANABII TANZANIA Mh.Dr.GeorDavie_SHOPRITE.


     Hata hivyo mara Baada ya Nabii Mkuu wa Karne ya 21 kutoka Tanzania Mh.Dr.GeorDavie kutamka maneno hayo ya kinabii Tulianza kuona uboreshaji wa Jiji La Arusha kuanza ambapo nyumba zilizo kuwa maeneo ya Kaloleni kuanza kubomolewa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kisasa zaidi.    (BOFYA HAPA).....   AU  (BOFYA HAPA)...
    Sanjari na hili Manispaa ya Jiji la Arusha iliweza kufanikiwa kuwatengea sehemu maalumu wafanya biashara wadogowadogo(machinga) sehemu ya kufanyia biashara zao kwa utaratibu maalu ikikumbukwa kuwa Muasisi wa Manabii Tanzania Mh.Dr. GeorDavie alitamka kuwa hata wafanya biashara wadogo watapata kufanya biashara zao kwa utulivu na kupata mawazo ya biashara bora zidi.(BOFYA HAPA)...

No comments:

Post a Comment