
Umoja wa mataifa umetoa wito ya
kuachiwa mara moja kwa watu 30, wa chama kikuu cha upinzani katika
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kutoka korokoroni.
Wanachama wa vyama vikuu viwili vya Union for Democracy na wenzao wa Social Progress, walikamatwa siku ya Jumapili katika mji wa Lubumbashi, ulioko Kusini mashariki mwa nchi hiyo, baada ya polisi kuvunja mkutano waliokuwa nao.
Utawala wa Rais, Joseph Kabila, umepiga marufuku mkutano wa aina yoyote wa kisiasa, pamoja na maandamano ya upinzani, tangu muda wake wa kuhudumu kama Rais kisheri, ulipomalizika mwaka mmoja uliopita.
Chama kingine cha upinzani- Union for the Congolese Nation, kimesema kwamba, kitajiondoa katika serikali ya ugawanaji mamlaka, kuhusiana na kucheleweshwa kwa uchaguzi mkuu.
Maandamano ya mara kwa mara ya upinzani nchini humo umekabiliwa vikali na utawala wa Rais Joseph Kabila.
No comments:
Post a Comment