Jamii nchini imetakiwa
kutambua mchango wa wazazi wao bila kujali kiwango cha msaada waliuopata kutoka
kwao.
Rai hiyo imetolewa na
kiongozi mkuu wa Huduma ya Ngurumo ya Upako Duniani Nabii Mkuu Mhe. Dr.
GeorDavie katika ibada ya jiji Chuo Kikuu
cha Manabii Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Nabii Mkuu DR.GEORDAVIE
amefafanua kuwa ipo tabia miongoni mwa
watu kuwalaumu wazazi kuwa hawajawandalia
msingi mzuri wa maisha jambo alilosema si sahihi na badala yake kwa kila anaye amini
nguvu ya huduma ya Ngurumo ya Upako anaweza kupokea kila anacho kihitaji.
Aidha katika ibada hiyo
Nabii Mkuu ametamka maneno mbalimbali ya hekima za kinabii na kusema wakati uwapo
katika nguvu ya kinabii hupaswi kuwalaumu wazazi hata kama
hawakuweza kukusaidia yale ambayo ulihitaji kutoka kwao, badala yake unapaswa
kuwashukuru wazazi kwa kukuzaa na pia kuchukua jukumu la kuwatunza na kuwasaidia kama wazazi wako.
Sanjari na hayo Nabii
Mkuu Dr Geordavie alitangaza kuwa wiki hii ni wiki ya wepesi katika majukumu
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment