Thursday, September 27, 2018

Kivuko cha MV Nyerere kilichokuwa kimepinduka na kuzama chainuliwa


Kivuko cha MV Nyerere kilichokuwa kimepinduka na kuzama kichwa chini, kimeinuliwa nakuwa wima kama kilivyokuwa hapo awali kabla ya ajali.

Zoezi hilo la kukinasua kivuko hicho  kilichonasa katika Ziwa Victoria Septemba 20,2018 limekuwa na mafanikio makubwa

Kivuko hicho kimenyanyuliwa baada ya jitihada za siku tano tangu Jumapili Septemba 23, 2018 zilizofanywa na wataalam wa uokoaji kutoka vyombo vya ulinzi na usalama wakiongozwa na maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Wataalam hao walikuwa wakifanya kazi ya kukinyanyua kivuko hicho usiku na mchana huku wakitumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupitisha maboya chini ya maji, kuyajaza upepo sambamba na kukifunga kamba kivuko hicho na kukivuta.

by rich voice

No comments:

Post a Comment