Kiongozi mkuu wa huduma ya Ngurumo ya upako duniani Mh Nabii
Mkuu Dr GeorDavie, amepata mualiko wa
heshma wa kushiriki katika hafla ya Jeshi
la polisi mkoani Arusha.
Mwaliko huu wa heshma ameupookea kutoka kwa kamishna msaidizi
mwandamizi wa jeshi la polisi ambaye pia ni kamandawa polisi mkoani Arusha
bwana Liberatus Sabas, mapema wiki hii.
Hafla hiyo itakayofanyika leo jioni itahusisha viongozi wa
kada mbalimbali ikiwemo viongozi wa kiserikali, lengo likiwa kuwakaribisha
maafisa wapya na kuwaaga wastaafu wa jeshi hilo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu ya Nabii Mkuu Mh Dr
GeorDavie, imeeleza kupokea taarifa hiyo, huku nabii mkuu akithibitisha
kuhudhuria hafla hiyo.
Jeshi la polisi mkoani Arusha limekuwa na utaratibu wa
kufanya halfa kila mwanzo wa mwaka lengo likiwa ni kuwakaribisha maafisa wapya
waliohamia katika mkoa wa Arusha kutoka mikoa mingine na kuwaaga wastaafu wa
jeshi hilo waliostaafu kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment